49
Zaburi 49
Upumbavu Wa Kutegemea Mali
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.
1 #
Isa 1:2; Za 33:8; 78:1 Sikieni haya, enyi mataifa yote,
sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.
2 #
Za 62:9
Wakubwa kwa wadogo,
matajiri na maskini pamoja:
3 #
Za 37:30; 119:130 Kinywa changu kitasema maneno ya hekima,
usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
4 #
Za 33:2; 78:2; 1Sam 16:16; Mit 1:6; Eze 12:22; 16:44; 18:2, 3; Hes 12:8; Lk 4:23 Nitatega sikio langu nisikilize mithali,
nitafafanua kitendawili kwa zeze:
5 #
Za 23:4; 27:1 Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja,
wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
6 #
Yer 48:7; Za 10:3; 73:12; Ay 22:25; 36:19 wale wanaotegemea mali zao
na kujivunia utajiri wao mwingi?
7 #
Mt 16:26
Hakuna mwanadamu awaye yote
awezaye kuukomboa uhai wa mwingine,
au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.
8 #
Hes 35:31; Mt 16:26; Ay 36:18 Fidia ya uhai ni gharama kubwa,
hakuna malipo yoyote yanayotosha,
9 #
Za 22:29; 89:48; 16:10; Ebr 9:27 ili kwamba aishi milele
na asione uharibifu.
10 #
Mhu 2:16, 18, 21; Za 92:6; 94:8; Ay 27:17; Lk 12:20 Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa;
wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia
na kuwaachia wengine mali zao.
11 #
Mk 5:3; Lk 8:27; Za 106:31; Kum 3:14 Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele,
makao yao vizazi vyote;
ingawa walikuwa na mashamba
na kuyaita kwa majina yao.
12 #
Ay 14:2
Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu;
anafanana na mnyama aangamiaye.
13 #
Lk 12:20
Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe,
pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.
14 #
Yer 43:11; Isa 14:2; Hes 16:30; Eze 31:14; Mal 4:3; Ay 21:13; Ufu 2:26; 1Kor 6:2; Za 9:17; 55:15; Dan 7:18, 22; Lk 22:30; 2Tim 2:12 Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini,#49:14 Kaburini hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu.
nacho kifo kitawala.
Wanyofu watawatawala asubuhi,
maumbile yao yataozea kaburini,
mbali na majumba yao makubwa ya fahari.
15 #
Za 56:13; Hos 13:14; Mwa 5:24 Lakini Mungu atakomboa uhai#49:15 Au: nafsi. wangu na kaburi,
hakika atanichukua kwake.
16Usitishwe mtu anapotajirika,
fahari ya nyumba yake inapoongezeka,
17 #
1Tim 6:7; Za 17:14 kwa maana hatachukua chochote atakapokufa,
fahari yake haitashuka pamoja naye.
18 #
Za 10:6; Lk 12:19 Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri,
na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,
19 #
Mwa 15:15; Ay 33:30 atajiunga na kizazi cha baba zake,
ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.
20 #
Mit 16:16; Mhu 3:19-21 Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu
ni kama wanyama waangamiao.