51
Zaburi 51
Kuomba Msamaha
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba.
1 #
2Sam 24:14; 12:13; Za 39:8; 86:15; 25:7; 119:88; 9:13; Neh 4:5; 9:27; Isa 63:7; Kol 2:14; 2Nya 6:23; Mdo 3:19 Ee Mungu, unihurumie,
kwa kadiri ya upendo wako usiokoma,
kwa kadiri ya huruma yako kuu,
uyafute makosa yangu.
2 #
Rum 3:3; Yer 2:22; 13:27; Mdo 22:16; Mit 20:30; Isa 4:4; Ebr 9:14; Zek 13:1; Ufu 1:5; 1Kor 6:11; Eze 13:1; 36:25; Mt 23:25, 26; 1Yn 1:7, 9 Unioshe na uovu wangu wote
na unitakase dhambi yangu.
3 #
Isa 59:12; Za 32:5 Kwa maana ninajua makosa yangu,
na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
4 #
1Sam 15:24; Mwa 20:6; Lk 15:21; Rum 3:4 Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi
na kufanya yaliyo mabaya machoni pako,
ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo,
na kuwa na haki utoapo hukumu.
5 #
Law 5:2; Ay 5:7; 14:4; Rum 5:12; Yn 3:6 Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi,
mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
6 #
Ay 9:4; 34:32; Za 119:66; 143:10 Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni,
ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.
7 #
Eze 36:25; Hes 19:6; Zek 13:1; Kut 12:22; Ebr 9:19; Isa 4:4; 1:19; 43:25; 44:22 Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi,
unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8 #
Isa 35:10; Kut 12:46; Yer 33:11; Yoe 1:16 Unipe kusikia furaha na shangwe,
mifupa uliyoiponda na ifurahi.
9 #
Yer 16:17; Zek 4:10; 2Sam 12:13 Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu,
na uufute uovu wangu wote.
10 #
Za 24:4; 78:37; Mt 5:8; Mdo 15:9; Eze 11:19; 18:31; 36:26; Mit 20:9; Yer 13:27; Efe 2:10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
11 #
Za 27:9; 138:8; 71:9; 106:3; Kut 33:15; Mwa 4:14; Isa 63:10; Eze 36:27; Efe 4:30; Rum 8:9 Usinitupe kutoka mbele zako
wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
12 #
Ay 33:26; Za 110:3; 18:35; Rum 8:15; 2Kor 3:17 Unirudishie tena furaha ya wokovu wako,
unipe roho ya utii, ili initegemeze.
13 #
Kut 33:13; Za 1:1; Mdo 9:21-22; Ay 33:27 Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako,
na wenye dhambi watakugeukia wewe.
14 #
2Sam 12:9; Za 5:8; 22:5; 39:8; 68:20; 88:1; 35:28; 71:15 Ee Mungu, Mungu uniokoaye,
niokoe na hatia ya kumwaga damu,
nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.
15 #
Kut 4:15
Ee Bwana, fungua midomo yangu,
na kinywa changu kitatangaza sifa zako.
16 #
1Sam 15:22
Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta,
hufurahii sadaka za kuteketezwa.
17 #
Mit 15:8; Hag 2:14; Mt 11:29 Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika,
moyo uliovunjika wenye toba,
Ee Mungu, hutaudharau.
18 #
Za 69:35; 147:2; 102:16; Zek 1:16-17; Isa 14:32; 44:26; 51:3; 51:19; Kum 33:19; Mal 3:3 Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi,
ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.
19Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki,
sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana,
pia mafahali watatolewa
madhabahuni mwako.