52
Zaburi 52
Hukumu Ya Mungu
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi. Baada ya Doegi, Mwedomu kumwendea Sauli na kumjulisha kuwa: “Daudi amekwenda nyumbani kwa Ahimeleki.”
1 #
Za 10:3; 44:8; 94:4; 1Sam 21:7 Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya?
Kwa nini unajivuna mchana kutwa,
wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?
2 #
Za 5:9; 59:7; Hes 6:5; Mit 12:18 Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.
Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.
3 #
Kut 10:10; Za 58:3; 1Sam 12:25; Amo 5:14, 15; Yn 3:20; Ufu 21:8; Yer 9:4, 5 Unapenda mabaya kuliko mema,
uongo kuliko kusema kweli.
4 #
Za 5:9; 10:7; 109:2; 120:2, 3; Mit 10:31; 12:19 Unapenda kila neno lenye kudhuru,
ewe ulimi wenye hila!
5 #
Kum 28:63; 29:28; Ay 28:13; 40:12; Isa 22:19; Mit 2:22; Eze 17:24 Hakika Mungu atakushusha chini
kwa maangamizi ya milele:
atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu
kutoka hema yako,
atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.
6 #
Ay 22:19; Za 58:10 Wenye haki wataona na kuogopa,
watamcheka, wakisema,
7 #
2Sam 22:3; Za 49:6; Mk 10:23; Mit 11:28; Ay 31:24, 25 “Huyu ni yule mtu ambaye
hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,
bali alitumainia wingi wa utajiri wake,
na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”
Neema Ya Mungu
8 #
Ufu 11:4; Za 1:3; 6:4; 13:5; 54:6 Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni
unaostawi katika nyumba ya Mungu,
nautegemea upendo wa Mungu usiokoma
milele na milele.
9 #
Ay 7:6; Za 16:3; 30:12; 25:3; 54:6; Kum 7:6 Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,
nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.
Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.