54
Zaburi 54
Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kutokana Na Adui
Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?”
1 #
1Sam 24:15; 20:1; 2Nya 20:6 Ee Mungu uniokoe kwa jina lako,
unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
2 #
Za 4:1; 5:1; 55:1 Ee Mungu, sikia maombi yangu,
usikilize maneno ya kinywa changu.
3 #
Za 36:1; 86:14; 18:48; 140:1, 4, 11; 1Sam 20:1 Wageni wananishambulia,
watu wakatili wanayatafuta maisha yangu,
watu wasiomjali Mungu.
4 #
1Nya 5:20; Za 20:2; 18:35; Isa 41:10; Ebr 13:6; Rum 8:31, 32 Hakika Mungu ni msaada wangu,
Bwana ndiye anayenitegemeza.
5 #
Kum 32:35; Isa 42:3; Mit 24:12; Za 89:49; 94:23 Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia,
kwa uaminifu wako uwaangamize.
6 #
Law 7:12, 16; Ezr 1:4; Za 27:6; 44:8; 52:9; 138:2; 142:7; 145:1; 69:30 Nitakutolea dhabihu za hiari;
Ee Bwana, nitalisifu jina lako
kwa kuwa ni vyema.
7Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote,
na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.