Zaburi 55
NEN

Zaburi 55

55
Zaburi 55
Maombi Ya Mtu Aliyesalitiwa Na Rafiki
Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi.
1 # Za 27:9; Mao 3:56 Ee Mungu, sikiliza maombi yangu,
wala usidharau hoja yangu.
2 # 1Sam 1:15-16; Za 4:1; 77:3; 86:6-7; 142:2 Nisikie na unijibu.
Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa
3 # 2Sam 16:6-8; 17:9; Za 143:3; 44:16; 71:11 kwa sauti ya adui,
kwa kukaziwa macho na waovu,
kwa sababu wananiletea mateso juu yangu
na kunitukana kwa hasira zao.
4 # Ay 18:11; Za 6:3; 102:3-5; Yn 12:27; Mt 26:37, 38; 2Kor 1:8-10 Moyo wangu umejaa uchungu,
hofu ya kifo imenishambulia.
5 # Ay 4:14; Eze 7:18; 2Kor 7:15; Isa 21:4; Kum 28:67; Yer 46:5; 49:5 Woga na kutetemeka vimenizunguka,
hofu kuu imenigharikisha.
6Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa!
Ningeruka niende mbali kupumzika.
7 # 1Sam 23:14 Ningalitorokea mbali sana
na kukaa jangwani,
8 # Za 31:20; 77:18; Isa 4:6; 25:4; 28:2; 29:6; 32:2 ningaliharakisha kwenda mahali pa salama,
mbali na tufani kali na dhoruba.”
9 # Mwa 4:17; 11:9; Mdo 2:4; Za 11:5; Isa 59:6; Yer 6:7; Eze 7:11; Hab 1:3 Ee Bwana, uwatahayarishe waovu
na uwachanganyishie semi zao,
maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.
10 # 1Pet 5:8 Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake,
uovu na dhuluma vimo ndani yake.
11 # Za 5:9; 10:7 Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini,
vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake.
12Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia,
kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu,
ningejificha asinione.
13 # 2Sam 15:12 Kumbe ni wewe, mwenzangu,
mshiriki na rafiki yangu wa karibu,
14 # Mdo 1:16-17; Za 42:4 ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,
tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.
15 # Za 64:7; 49:14; Mit 6:5; Isa 29:5; 47:9, 11; 1The 5:3; Hes 16:30 Kifo na kiwajie adui zangu ghafula,
na washuke kuzimu wangali hai,
kwa maana uovu upo ndani yao.
16Lakini ninamwita Mungu,
naye Bwana huniokoa.
17 # Za 141:2; 88:13; 92:2; 5:3; Mdo 3:1; 10:9; 10:3, 30; Lk 18:1; Dan 6:10 Jioni, asubuhi na adhuhuri
ninalia kwa huzuni,
naye husikia sauti yangu.
18 # 2Nya 32:7 Huniokoa nikawa salama katika vita
vilivyopangwa dhidi yangu,
ingawa watu wengi hunipinga.
19 # Kum 33:27; Za 29:10; 78:59; 36:1; 64:4; Kut 15:18 Mungu anayemiliki milele,
atawasikia na kuwaadhibu,
watu ambao hawabadilishi njia zao,
wala hawana hofu ya Mungu.
20 # Za 7:4; 41:9 Mwenzangu hushambulia rafiki zake,
naye huvunja agano lake.
21 # Za 59:7; 57:4; 12:2; 64:3; Ufu 1:16; Mit 5:3; 6:24; 12:18 Mazungumzo yake ni laini kama siagi,
hata hivyo vita vimo moyoni mwake.
Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,
hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
22 # 1Pet 5:7; Za 15:5; 18:35; 112:6; 21:7; 37:24; Mt 6:25-34 Mtwike Bwana fadhaa zako,
naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
23 # Za 5:6; 11:1; 9:15; 73:18; 94:13; 25:2; 30:3; 56:3; Isa 14:15; Eze 28:8; Lk 8:31; Ay 15:32 Lakini wewe, Ee Mungu,
utawashusha waovu katika shimo la uharibifu.
Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila,
hawataishi nusu ya siku zao.
Lakini mimi ninakutumaini wewe.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014