Zaburi 57
NEN

Zaburi 57

57
Zaburi 57
Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Baada ya kumponyoka Sauli pangoni.
1 # Isa 26:20 Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie,
kwa maana nafsi yangu inakukimbilia.
Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia
mpaka maafa yapite.
2 # Za 138:8 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana,
Mungu atimizaye makusudi yake kwangu.
3 # Za 18:9, 16; 69:14; 142:5, 7; 56:1; 25:10; 40:11; 115:1 Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa,
akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali;
Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake.
4 # Za 35:17; 55:21; 64:3; Mit 30:14 Niko katikati ya simba,
nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu:
watu ambao meno yao ni mikuki na mishale,
ambao ndimi zao ni panga kali.
5 # Za 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
utukufu wako na uenee duniani kote.
6 # Es 6:13; Za 31:4; 9:15; 140:5; 7:15; 38:6; 10:9; 145:14; Mit 28:10; Mhu 10:8 Waliitegea miguu yangu nyavu,
nikainamishwa chini na dhiki.
Wamechimba shimo katika njia yangu,
lakini wametumbukia humo wao wenyewe.
7 # Za 112:7; 108:1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;
nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.
8 # Za 33:2; 149:3; 150:3; Amu 5:12 Amka, nafsi yangu!
Amka, kinubi na zeze!
Nitayaamsha mapambazuko.
9Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;
nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.
10 # Za 36:5; 108:4 Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni,
uaminifu wako unazifikia anga.
11 # Za 8:1; 149:3; 150:3; Amu 5:12 Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni,
utukufu wako na uwe duniani pote.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014