Zaburi 59
NEN

Zaburi 59

59
Zaburi 59
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue.
1 # Za 82:2 # Za 143:9; 20:1 Ee Mungu, uniokoe na adui zangu,
unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.
2 # Za 14:4; 36:12; 53:4; 92:7; 94:16; 26:9; 139:19; Mit 29:10 Uniponye na watu watendao mabaya,
uniokoe kutokana na wamwagao damu.
3 # Za 56:6; 1Sam 26:18 Tazama wanavyonivizia!
Watu wakali wananifanyia hila,
ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea
wala kutenda dhambi.
4 # Za 13:3; 119:3; Mt 5:11 Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia.
Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya!
5 # Za 69:6; 80:4; 84:8; 44:23; 9:5; Isa 10:3; Yer 18:23; Dan 4:35 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli!
Zinduka uyaadhibu mataifa yote,
usionyeshe huruma kwa wasaliti.
6 # Za 22:16 Hurudi wakati wa jioni,
wakibweka kama mbwa,
wakiuzurura mji.
7 # Za 55:21; 94:4; Mit 10:32; 12:23; 15:2, 28; Ay 22:13 Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao,
hutema upanga kutoka midomo yao,
nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”
8 # Za 2:4; 37:13; Mit 1:26 Lakini wewe, Bwana, uwacheke;
unayadharau mataifa hayo yote.
9 # Za 18:1; 9:9; 18:2; 62:2; 71:3 Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe,
wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,
10Mungu wangu unipendaye.
Mungu atanitangulia,
naye atanifanya niwachekelee
wale wanaonisingizia.
11 # Kum 4:9; 6:12; Za 3:3; 84:9; 89:10; 106:27; 144:6; Isa 33:3; Mwa 4:12, 13 Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu,
au sivyo watu wangu watasahau.
Katika uwezo wako wafanye watangetange
na uwashushe chini.
12 # Za 10:7; 64:8; Mit 10:14; 12:13; Isa 2:12; 5:15; Sef 3:11 Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao,
kwa ajili ya maneno ya midomo yao,
waache wanaswe katika kiburi chao.
Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,
13 # Za 83:18; 104:35 wateketeze katika ghadhabu,
wateketeze hadi wasiwepo tena.
Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia
kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo.
14Hurudi jioni,
wakibweka kama mbwa,
wakiuzurura mji.
15 # Ay 15:23 Wanatangatanga wakitafuta chakula,
wasipotosheka hubweka kama mbwa.
16 # Za 5:3; 88:13; 101:1; 108:1; 1Sam 2:10; 2Sam 22:3; Kum 4:30 Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,
asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;
kwa maana wewe ndiwe ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa shida.
17 # Za 59:1 Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.
Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,
Mungu unipendaye.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014