60
Zaburi 60
Kuomba Kuokolewa
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi.
1 #
2Sam 5:20; Za 18:7; 44:9; 79:5; 80:3; 60:2; 2Nya 7:14 Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu,
umekasirika: sasa turejeshe upya!
2Umetetemesha nchi na kuipasua;
uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka.
3 #
Za 71:20; 75:8; Isa 29:9; 51:17; 63:6; Yer 25:16; Zek 12:2; Ufu 14:10 Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa;
umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha.
4 #
Isa 5:26; 11:10, 12; 18:3 Kwa wale wanaokucha wewe,
umewainulia bendera,
ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde.
5 #
Ay 40:14; Kum 33:12; Za 108:6 Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,
ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
6 #
Mwa 12:6; 33:17; Za 89:35; Yos 13:27 Mungu amenena kutoka patakatifu pake:
“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi
na kulipima Bonde la Sukothi.
7 #
Yos 13:31; Hes 34:19; Mwa 41:52; 49:10; Kum 33:17 Gileadi ni yangu na Manase ni yangu;
Efraimu ni kofia yangu ya chuma,
nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
8 #
2Sam 8:1
Moabu ni sinia langu la kunawia,
juu ya Edomu natupa kiatu changu;
nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?
Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
10 #
Yos 7:12; Za 44:9 Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,
na hutoki tena na majeshi yetu?
11 #
Za 146:3; Mit 3:5 Tuletee msaada dhidi ya adui,
kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
12 #
1Nya 19:13; Ay 40:12; Za 44:5 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,
naye atawaponda adui zetu.