61
Zaburi 61
Kuomba Ulinzi
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 64:1; 4:1; 86:6 Ee Mungu, sikia kilio changu,
usikilize maombi yangu.
2 #
Za 6:2; 18:2; 31:2; 94:22; 1Tim 2:8 Kutoka miisho ya dunia ninakuita,
ninaita huku moyo wangu unadhoofika;
uniongoze kwenye mwamba
ule ulio juu kuliko mimi.
3 #
Za 9:9; 46:1; 62:7; 59:9; Mit 18:10 Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu,
ngome imara dhidi ya adui.
4 #
Kum 32:11; Mt 23:37; Ufu 3:12; Za 15:1; 23:6 Natamani kukaa hemani mwako milele,
na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.
5 #
Hes 30:2; Kut 6:3; Neh 1:11; Mt 6:9; Za 56:12; 102:15; Isa 59:19; 1Kor 3:21-23; Kum 33:9 Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu,
umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.
6 #
1Fal 3:14; Za 21:4 Mwongezee mfalme siku za maisha yake,
miaka yake kwa vizazi vingi.
7 #
Za 40:11; 41:12; Lk 22:69; Efe 1:20; Kol 3:1; Lk 1:32 Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele;
amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.
8 #
Kut 15:1; Hes 30:2; Kum 23:21; Za 7:17; 30:4; 56:12 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako
na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.