62
Zaburi 62
Mungu Kimbilio La Pekee
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 5:3
Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko;
wokovu wangu watoka kwake.
2 #
Kut 15:2; Za 18:31; 89:26; 59:9; Ay 29:18 Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;
yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.
3 #
Isa 30:13
Mtamshambulia mtu hata lini?
Je, ninyi nyote mtamtupa chini,
ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika?
4 #
Za 28:3; 55:21 Walikusudia kikamilifu kumwangusha
toka mahali pake pa fahari;
wanafurahia uongo.
Kwa vinywa vyao hubariki,
lakini ndani ya mioyo yao hulaani.
5 #
Mik 7:7, 10; Za 62:1 Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,
tumaini langu latoka kwake.
6Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;
ndiye ngome yangu, sitatikisika.
7 #
Za 61:3
Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,
ndiye mwamba wangu wenye nguvu
na kimbilio langu.
8 #
Isa 26:4; 1Sam 1:15; Za 37:5; 42:4; Mt 26:36-46 Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote,
miminieni mioyo yenu kwake,
kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.
9 #
Za 49:2; Ay 7:7; Isa 40:15 Binadamu wa ngazi ya chini ni pumzi tu,
nao wa ngazi ya juu ni uongo tu;
wakipimwa kwenye mizani, si chochote;
wote kwa pamoja ni pumzi tu.
10 #
Za 12:5; Isa 61:8; 26:4; 1Tim 6:17; Eze 22:29; Nah 3:1; Lk 12:15; Ay 31:25; Mt 19:23, 24; 1Tim 6:6-10; Mk 10:23 Usitumainie vya udhalimu
wala usijivune kwa vitu vya wizi;
ingawa utajiri wako utaongezeka,
usiviwekee moyo wako.
11 #
1Nya 29:11; Ufu 19:1 Jambo moja Mungu amelisema,
mambo mawili nimeyasikia:
kwamba, Ee Mungu,
wewe una nguvu,
12 #
Za 130:7; 103:8; 86:5; 28:4; Ay 21:31; Mt 16:27; Rum 2:6; 1Kor 3:8; Kol 3:25; 1Pet 1:17 na kwamba, Ee Bwana,
wewe ni mwenye upendo.
Hakika utampa kila mtu thawabu
kwa kadiri ya alivyotenda.