Zaburi 63
NEN

Zaburi 63

63
Zaburi 63
Shauku Kwa Ajili Ya Uwepo Wa Mungu
Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda.
1 # Za 42:2; 84:2; 143:6 Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,
nakutafuta kwa moyo wote;
nafsi yangu inakuonea kiu,
mwili wangu unakuonea wewe shauku,
katika nchi kame na iliyochoka
mahali ambapo hapana maji.
2 # Za 15:1; 27:4; 68:24; Kut 16:7; 1Nya 16:11 Nimekuona katika mahali patakatifu
na kuuona uwezo wako na utukufu wako.
3 # Isa 30:13; Yn 3:16; Za 36:7; 69:16; 106:45; 109:21 Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,
midomo yangu itakuadhimisha.
4 # Za 28:3; 104:33; 146:2; Isa 38:20; 1Tim 2:8 Nitakusifu siku zote za maisha yangu,
na kwa jina lako nitainua mikono yangu.
5 # Za 17:15; 36:8; Mt 5:6; Isa 25:6 Nafsi yangu itatoshelezwa
kama kwa wingi wa vyakula;
kwa midomo iimbayo
kinywa changu kitakusifu wewe.
6 # Kum 6:4-9; Za 119:148; 16:7; 140:5; Mt 14:25 Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe,
ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
7 # Za 27:9; 118:7; Rum 2:12; Isa 26:9 Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,
chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.
8 # Hes 32:12; Hos 6:3; Isa 26:9; Za 41:12 Nafsi yangu inaambatana nawe,
mkono wako wa kuume hunishika.
9 # Za 40:14; 55:15; 71:20; 95:4; 139:15 Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa,
watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.
10 # Yer 18:21; Eze 35:5; Amo 1:11; Mao 5:18 Watatolewa wafe kwa upanga,
nao watakuwa chakula cha mbweha.
11 # Sef 1:5; Isa 19:18; 45:23; 65:16; Ay 5:16; Rum 3:19 Bali mfalme atafurahi katika Mungu,
wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,
bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014