Zaburi 66
NEN

Zaburi 66

66
Zaburi 66
Kusifu Mungu Kwa Ajili Ya Wema Wake
Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi.
1 # Za 81:1; 84:8; 98:4; 100:1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote!
2 # Za 79:9; 86:9; Isa 42:8, 12; 43:21 Imbeni utukufu wa jina lake;
mpeni sifa zake kwa utukufu!
3 # Kum 7:21; 10:21; Za 106:22; 111:6; 18:44; 65:5; 145:6; 2Sam 22:45 Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako!
Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba
adui wananyenyekea mbele zako.
4 # Za 22:27; 7:17; 67:3 Dunia yote yakusujudia,
wanakuimbia wewe sifa,
wanaliimbia sifa jina lako.”
5 # Za 66:3; 46:8; 106:22 Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda,
mambo ya kutisha aliyoyatenda
miongoni mwa wanadamu!
6 # Mwa 8:1; Kut 14:21, 22; Law 23:40; Yos 3:14; Za 78:13; Isa 63:13, 14; 1Kor 10:1 Alifanya bahari kuwa nchi kavu,
wakapita kati ya maji kwa miguu,
njooni, tumshangilie.
7 # Kut 15:18; 3:16; Hes 17:10; Za 11:4; 112:10; 140:8; 145:13 Yeye hutawala kwa uwezo wake milele,
macho yake huangalia mataifa yote:
waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake.
8 # Za 22:23 Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu,
sauti ya sifa yake isikike,
9 # Za 30:3; Kum 32:35; Ay 12:5 ameyahifadhi maisha yetu
na kuizuia miguu yetu kuteleza.
10 # Kut 15:25; Ay 6:29; 28:1; Za 12:6; Zek 13:9 Ee Mungu, wewe ulitujaribu,
ukatusafisha kama fedha.
11 # Za 38:4; 142:7; 146:7; Isa 61:1; 10:27; 42:7, 22; Mwa 3:17; Kut 1:14 Umetuingiza kwenye nyavu
na umetubebesha mizigo mizito
migongoni mwetu.
12 # Isa 51:13; Za 18:19 Uliwaruhusu watu watukalie vichwani,
tulipita kwenye moto na kwenye maji,
lakini ulituleta kwenye nchi
iliyojaa utajiri tele.
13 # Za 51:19; 22:25; 50:14; 116:14; Mhu 5:4; Yon 2:9 Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa
na kukutimizia nadhiri zangu:
14nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi
na nilizotamka kwa kinywa changu
nilipokuwa katika shida.
15 # Law 16:5; Za 51:19 Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono
na sadaka za kondoo dume,
nitakutolea mafahali na mbuzi.
16 # Za 34:11; 71:15, 24 Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu,
nami niwaambie aliyonitendea.
17Nilimlilia kwa kinywa changu,
sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu.
18 # Kum 1:45; 1Sam 8:18; Yak 4:3; Isa 1:15; Ay 11:14, 15; Mit 15:29 Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu,
Bwana asingekuwa amenisikiliza;
19 # Za 18:6 lakini hakika Mungu amenisikiliza
na amesikia sauti yangu katika maombi.
20 # Za 22:24 Sifa apewe Mungu,
ambaye hakulikataa ombi langu
wala kunizuilia upendo wake!

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014