67
Zaburi 67
Mataifa Yahimizwa Kumsifu Mungu
Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo.
1 #
Hes 6:24-26; Za 4:6; 31:16; 119:135; 2Kor 4:6 Mungu aturehemu na kutubariki,
na kutuangazia nuru za uso wake,
2 #
Isa 40:5; 52:10; 62:1, 2; Lk 2:30-32; Tit 2:11; Za 98:2; Mdo 10:35; 13:10 ili njia zako zijulikane duniani,
wokovu wako katikati ya mataifa yote.
3 #
Za 67:5; Isa 24:15, 16 Ee Mungu, mataifa na wakusifu,
mataifa yote na wakusifu.
4 #
Za 100:1-2; 9:4; 96:10-13; 68:32 Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe,
kwa kuwa unatawala watu kwa haki
na kuongoza mataifa ya dunia.
5 #
Za 67:3
Ee Mungu, mataifa na wakusifu,
mataifa yote na wakusifu.
6 #
Mwa 8:22; 12:2; Law 26:4; Za 85:12; Isa 55:10; Eze 34:27; Zek 8:12 Ndipo nchi itatoa mazao yake,
naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.
7 #
Za 2:8; 33:8 Mungu atatubariki
na miisho yote ya dunia itamcha yeye.