68
Zaburi 68
Wimbo Wa Taifa Wa Shangwe Kwa Ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.
1 #
Za 89:10; 132:8; 12:5; 18:14; 92:9; 144:6; Hes 10:35; Isa 17:13; 21:15; 33:3 Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike,
adui zake na wakimbie mbele zake.
2 #
Za 37:20; 80:16; 22:14; 9:3; Hes 10:35 Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo,
vivyo hivyo uwapeperushe mbali,
kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto,
vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu.
3 #
Za 64:10; 97:12 Bali wenye haki na wafurahi,
washangilie mbele za Mungu,
wafurahi na kushangilia.
4 #
2Sam 22:50; Za 7:17; 30:4; 66:2; 68:33; 96:2; 100:4; 135:3; 83:18; Kut 6:3; 20:21; Kum 33:26 Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake,
mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu:
jina lake ni Bwana,
furahini mbele zake.
5 #
Za 10:14; Kut 22:22; Kum 10:18; 26:15; Yer 25:30 Baba wa yatima, mtetezi wa wajane,
ni Mungu katika makao yake matakatifu.
6 #
Lk 4:18; Za 146:7; 113:9; 102:20; 79:11; 25:16; Isa 58:11; 35:7; 49:10; 61:1 Mungu huwaweka wapweke katika jamaa,
huwaongoza wafungwa wakiimba,
bali waasi huishi katika nchi kame.
7 #
Kut 13:21; Za 78:40; 106:14 Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako,
ulipopita nyikani,
8 #
2Sam 22:8; Amu 5:4, 5; Mhu 11:3; 2Sam 21:10; Kum 33:2 dunia ilitikisika,
mbingu zikanyesha mvua,
mbele za Mungu, Yule wa Sinai,
mbele za Mungu, Mungu wa Israeli.
9 #
Kum 32:2; Ay 36:28; Eze 34:26 Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi
na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka.
10 #
Kum 28:12; Za 65:9 Ee Mungu, watu wako waliishi huko,
nawe kwa wingi wa utajiri wako
uliwapa maskini mahitaji yao.
11 #
Lk 2:13
Bwana alitangaza neno,
waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:
12 #
Yos 10:16; Amu 5:30 “Wafalme na majeshi walikimbia upesi,
watu waliobaki kambini waligawana nyara.
13 #
Mwa 49:14
Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini,
mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha,
manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.”
14 #
2Sam 22:15; Amu 9:48 Wakati Mwenyezi#68:14 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. alipowatawanya wafalme katika nchi,
ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni.
15Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka,
milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka.
16 #
Za 132:13, 14; 2:6; Kum 12:5 Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka,
kwa nini mnakazia macho kwa wivu,
katika mlima Mungu anaochagua kutawala,
ambako Bwana mwenyewe ataishi milele?
17 #
2Fal 2:11; Isa 66:15; Hab 3:8; Dan 7:10 Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu,
na maelfu ya maelfu;
Bwana amekuja kutoka Sinai
hadi katika patakatifu pake.
18 #
Za 47:5; 7:7; Amu 5:12; Efe 4:8; Hes 17:10 Ulipopanda juu, uliteka mateka,
ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu,
hata kutoka kwa wale walioasi,
ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko.
19 #
Za 65:5; 81:6 Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu,
ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.
20 #
1Sam 10:19; Za 56:13; Yer 45; 5; Eze 6:8 Mungu wetu ni Mungu aokoaye,
Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo.
21 #
Za 74:14; 110:5; Hab 3:13 Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake,
vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi.
22 #
Ay 36:30; Mt 18:6 Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani;
nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari,
23 #
Za 58:10; 1Fal 21:19; 2Fal 9:36 ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako,
huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.”
24 #
Za 63:2
Ee Mungu, maandamano yako yameonekana,
maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu,
yakielekea patakatifu pake.
25 #
1Nya 15:16; 6:31; 2Nya 5:12; Ufu 18:22; Mwa 31:27; Isa 5:12 Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda,
pamoja nao wako wanawali wakipiga matari.
26 #
Za 22:22; Ebr 2:12; Law 19:2 Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa,
msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli.
27 #
1Sam 9:21; Hes 34:21; Amu 5:18 Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza,
wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda,
hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali.
28 #
Kut 9:16; Za 29:11; Isa 26:12; 29:23; 45:11; 60:21; 64:8 Ee Mungu, amuru uwezo wako,
Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako,
kama ulivyofanya hapo awali.
29 #
2Nya 9:24; 32:23 Kwa sababu ya Hekalu lako Yerusalemu
wafalme watakuletea zawadi.
30 #
Isa 27:1; 34:7; 51:9; Ay 40:21; Eze 29:3; Za 22:12; 18:14; 120:7; 89:10; 140:2; Yer 50:27 Mkemee mnyama aliyeko kwenye manyasi,
kundi la mafahali katikati ya ndama za mataifa.
Na walete minara ya madini ya fedha wakinyenyekea.
Tawanya mataifa yapendayo vita.
31 #
Isa 19:19; 43:3; 45:14; 11:11; 18:1; Sef 3:10 Wajumbe watakuja kutoka Misri,
Kushi#68:31 Kushi hapa ina maana maeneo ya Naili ya juu, yaani Ethiopia. atajisalimisha kwa Mungu.
32 #
Za 46:6; 67:4; 7:17 Mwimbieni Mungu, enyi falme za dunia,
mwimbieni Bwana sifa,
33 #
Kum 33:26; Kut 9:23; Za 29:3, 4; Isa 30:30; 33:3; 66:6; 45:3 mwimbieni sifa yeye apandaye mbingu za kale zilizo juu,
yeye angurumaye kwa sauti kuu.
34 #
Za 68:28; 45:3 Tangazeni uwezo wa Mungu,
ambaye fahari yake iko juu ya Israeli,
ambaye uwezo wake uko katika anga.
35 #
Mwa 28:17; Isa 40:29; 41:10; 50:2; Za 66:20; 18:1; 29:11; 28:6; 2Kor 1:3; Kum 7:21 Ee Mungu, wewe unatisha katika mahali patakatifu pako,
Mungu wa Israeli huwapa watu wake uwezo na nguvu.
Mungu Asifiwe!