69
Zaburi 69
Kilio Cha Kuomba Msaada Wakati Wa Dhiki
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 42:7; 32:6; Yon 2:5 Ee Mungu, niokoe,
kwa maana maji yamenifika shingoni.
2 #
Ay 30:19
Ninazama kwenye vilindi vya matope,
pasipo mahali pa kukanyaga,
Nimefika kwenye maji makuu,
mafuriko yamenigharikisha.
3 #
Za 6:6; 119:82 Nimechoka kwa kuomba msaada,
koo langu limekauka.
Macho yangu yanafifia,
nikimtafuta Mungu wangu.
4 #
Yn 15:25; Za 25:19; 35:19; 38:19; 40:14; 119:95; Isa 32:7 Wale wanaonichukia bila sababu
ni wengi kuliko nywele za kichwa changu;
wengi ni adui kwangu bila sababu,
wale wanaotafuta kuniangamiza.
Ninalazimishwa kurudisha
kitu ambacho sikuiba.
5 #
Za 38:5; 44:21 Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu,
wala hatia yangu haikufichika kwako.
6Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote,
wakutumainio wasiaibishwe
kwa ajili yangu;
wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu,
Ee Mungu wa Israeli.
7 #
Yer 15:15; Za 39:8; 44:15 Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako,
aibu imefunika uso wangu.
8 #
Ay 19:13-15; Za 31:11; 38:11; Isa 53:3; Yn 7:5 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,
mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.
9 #
Yn 2:17; Rum 15:3; Za 89:50-51 Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila,
matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.
10 #
Za 35:13
Ninapolia na kufunga,
lazima nivumilie matusi.
11 #
2Sam 3:31; Za 35:13 Ninapovaa nguo ya gunia,
watu hunidharau.
12 #
Mwa 18:1; 23:10; Ay 30:9 Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga,
nimekuwa wimbo wa walevi.
13 #
Isa 49:8; 2Kor 6:2; Za 17:7; 51:1 Lakini Ee Bwana, ninakuomba,
kwa wakati ukupendezao;
katika upendo wako mkuu, Ee Mungu,
unijibu kwa wokovu wako wa hakika.
14 #
Za 69:2; 144:7 Uniokoe katika matope,
usiniache nizame;
niokoe na hao wanichukiao,
kutoka kwenye vilindi vya maji.
15 #
Za 36:6; 68:22; Hes 21:33; Yer 22:20 #
Za 28:1; 124:4, 5; Hes 16:33 Usiache mafuriko yanigharikishe
au vilindi vinimeze,
au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.
16 #
Za 63:3
Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako;
kwa huruma zako nyingi unigeukie.
17 #
Za 22:24; 143:7; 50:15; 66:14 Usimfiche mtumishi wako uso wako,
uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.
18 #
Za 49:15
Njoo karibu uniokoe,
nikomboe kwa sababu ya adui zangu.
19 #
Za 22:6
Unajua jinsi ninavyodharauliwa,
kufedheheshwa na kuaibishwa,
adui zangu wote unawajua.
20 #
Ay 16:2; Isa 63:5; Za 142:4 Dharau zimenivunja moyo
na nimekata tamaa,
nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata,
wa kunituliza, lakini sikumpata.
21 #
Hes 6:3; Lk 23:36; Mt 27:34, 48; Mk 15:23, 36; Yn 19:28-30 Waliweka nyongo katika chakula changu
na walinipa siki nilipokuwa na kiu.
22 #
1Sam 28:9; Ay 18:10 Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego,
nayo iwe upatilizo na tanzi.
23 #
Rum 11:9-10
Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,
nayo migongo yao iinamishwe daima.
24 #
Za 79:6; Yer 10:25 Uwamwagie ghadhabu yako,
hasira yako kali na iwapate.
25 #
Law 26:43; Mt 23:38; Mdo 1:20 Mahali pao na pawe ukiwa,
wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.
26 #
Ay 19:22; Zek 1:15 Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi,
na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.
27 #
Neh 4:5; Za 109:14 Walipize uovu juu ya uovu,
usiwaache washiriki katika wokovu wako.
28 #
Kut 32:32-33; Lk 10:20; Eze 13:9 Wafutwe kutoka kitabu cha uzima
na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.
29 #
Za 20:1
Mimi niko katika maumivu na dhiki;
Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.
30 #
Za 28:7; 34:3 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
31 #
Za 50:9-13; 51:16 Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume,
zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.
32 #
Za 34:2; 22:26 Maskini wataona na kufurahi:
ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!
33 #
Za 12:5
Bwana huwasikia wahitaji
wala hadharau watu wake waliotekwa.
34 #
Za 96:11; 98:7; Isa 44:23 Mbingu na dunia zimsifu,
bahari na vyote viendavyo ndani yake,
35 #
Oba 1:17; Ezr 9:9; Za 51:18 kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni
na kuijenga tena miji ya Yuda.
Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,
36 #
Za 25:13; 37:29 watoto wa watumishi wake watairithi
na wale wote walipendao jina lake
wataishi humo.