Zaburi 70
NEN

Zaburi 70

70
Zaburi 70
Kuomba Msaada
(Zaburi 40:13-17)
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.
1 # Za 35:4; 6:10; 35:26; 71:12; 109:29; 129:5 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
2 # Za 35:2 Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4 # Za 31:6, 7; 35:27; 32:11; 118:24; 9:10 Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!”
5 # Za 109:22; 141:1; 30:10; 86:1; 33:10; 18:2; 119:60 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana, usikawie.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014