71
Zaburi 71
Kuomba Ulinzi Na Msaada Siku Zote Za Maisha
1 #
Kum 23:15; Rut 2:12; Za 22:5 Ee Bwana, nimekukimbilia wewe,
usiache nikaaibika kamwe.
2 #
2Fal 19:16
#
Kut 34:6
Kwa haki yako uniponye na kuniokoa,
unitegee sikio lako uniokoe.
3 #
Za 18:2
Uwe kwangu mwamba wa kimbilio,
mahali nitakapokimbilia kila wakati;
toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe
ni mwamba wangu na ngome yangu.
4 #
2Fal 19:19; Za 140:4; Mwa 48:16 Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu,
kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.
5 #
Za 9:18; 25:5; Ay 4:6; Yer 17:7 Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi,
tegemeo langu tangu ujana wangu.
6 #
Ay 3:16; Za 9:1; 22:9; 34:1; 52:9; 119:164; 145:2 Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe,
ulinitoa tumboni mwa mama yangu.
Nitakusifu wewe daima.
7 #
Kum 28:46; 1Kor 4:9; Za 61:3; 2Sam 22:3 Nimekuwa kama kioja kwa wengi,
lakini wewe ni kimbilio langu imara.
8 #
Za 71:15; 51:15; 63:5; 96:6; 104:1 Kinywa changu kimejazwa sifa zako,
nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.
9 #
Za 51:11; 92:14; Kum 4:31; 31:6 Usinitupe wakati wa uzee,
wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.
10 #
Za 3:7; 10:8; 59:3; 31:13; Mt 1:10; 12:14 Kwa maana adui zangu wananisengenya,
wale wanaonivizia kuniua wafanya hila.
11 #
Isa 40:27; 54:7; Mt 27:46; Za 7:2; 9:10; Mao 5:20 Wanasema, “Mungu amemwacha,
mkimbilieni mkamkamate,
kwani hakuna wa kumwokoa.”
12 #
Za 38:21, 22; 22:19 Ee Mungu, usiwe mbali nami,
njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.
13 #
Ay 8:22; Za 15:3; 70:2; Yer 18:19 Washtaki wangu na waangamie kwa aibu,
wale wanaotaka kunidhuru
na wafunikwe kwa dharau na fedheha.
14 #
Za 25:3; 42:5; 130:7; 131:3 Lakini mimi, nitatumaini siku zote,
nitakusifu zaidi na zaidi.
15 #
Za 71:8; 66:6; 51:14 Kinywa changu kitasimulia haki yako,
wokovu wako mchana kutwa,
ingawa sifahamu kipimo chake.
16 #
Za 77:12; 106:2; 118:15; 9:1; 145:4 Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja
na kutangaza matendo yako makuu,
nitatangaza haki yako, yako peke yako.
17 #
Yer 7:13; Ay 5:9; Za 26:7; 86:10; 96:3; Kum 4:5 Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu,
hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu.
18 #
Isa 46:4; Kut 9:16; Ay 8:8; Yoe 1:3; Za 78:4; 145:4; 22:30, 31 Ee Mungu, usiniache,
hata niwapo mzee wa mvi,
mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho,
nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.
19 #
Lk 1:49; Za 36:5; 35:10; 77:13; 89:8; 126:2 Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu,
wewe ambaye umefanya mambo makuu.
Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?
20 #
Za 80:3, 19; 25:17; 85:4; 63:9; Hos 6:2 Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu,
utanihuisha tena,
kutoka vilindi vya dunia
utaniinua tena.
21 #
Za 18:35; 86:17; Isa 12:1; 40:1, 2; 49:13; 54:10 Utaongeza heshima yangu
na kunifariji tena.
22 #
Za 33:2; 92:3; 144:9; Ay 21:12; 2Fal 19:22 Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi
kwa ajili ya uaminifu wako;
Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli,
nitakuimbia sifa kwa zeze.
23 #
Za 20:5; Kut 15:13 Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha
ninapokuimbia sifa,
mimi, ambaye umenikomboa.
24 #
Za 35:28; Es 9:2 Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki
mchana kutwa,
kwa maana wale waliotaka kunidhuru,
wameaibishwa na kufadhaishwa.