72
Zaburi 72
Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme
Zaburi ya Solomoni.
1 #
Kum 1:16; Za 9:8 Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,
mwana wa mfalme kwa haki yako.
2 #
Isa 11:2, 4, 5; 16:5; 9:7; Yer 23:5; 33:15 Atawaamua watu wako kwa haki,
watu wako walioonewa kwa haki.
3Milima italeta mafanikio kwa watu,
vilima tunda la haki.
4 #
Za 27:11; 76:9; 9:12; Isa 49:13; 11:4; 29:19; 32:7 Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu
na atawaokoa watoto wa wahitaji,
ataponda mdhalimu.
5 #
1Sam 13:13; Za 33:11 Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.
6 #
Kum 32:2
Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,
kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
7 #
Za 92:12; Mit 14:11 Katika siku zake wenye haki watastawi;
mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
8 #
Kut 23:31; 1Fal 4:21; Zek 9:10 Atatawala kutoka bahari hadi bahari
na kutoka Mto#72:8 Yaani Mto Frati. mpaka miisho ya dunia.
9Makabila ya jangwani watamsujudia,
na adui zake wataramba mavumbi.
10 #
Mwa 10:4, 7; Es 10:1; 1Fal 9:16; 2Nya 9:24 Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali
watamletea kodi;
wafalme wa Sheba na Seba
watampa zawadi.
11 #
Mwa 27:29; Ezr 1:2 Wafalme wote watamsujudia
na mataifa yote yatamtumikia.
12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,
aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
13 #
Isa 60:10; Yoe 2:18; Lk 10:33 Atawahurumia wanyonge na wahitaji
na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
14 #
Za 69:18; Eze 13:23; 34:10; 1Sam 26:21 Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,
kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
15 #
Mwa 10:7; Za 35:28 Aishi maisha marefu!
Na apewe dhahabu ya Sheba.
Watu wamwombee daima
na kumbariki mchana kutwa.
16 #
Eze 34:27; Isa 4:2; 27:6; 44:4; 58:11; 66:14; Mwa 27:18; Hes 22:4; Za 4:7; 92:12; 104:16 Nafaka ijae tele katika nchi yote,
juu ya vilele vya vilima na istawi.
Tunda lake na listawi kama Lebanoni,
listawi kama majani ya kondeni.
17 #
Kut 3:15; Lk 1:48; Za 89:36; Mwa 12:3 Jina lake na lidumu milele,
na lidumu kama jua.
Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,
nao watamwita aliyebarikiwa.
18 #
1Nya 29:10; Za 41:13; 106:48; Lk 1:68; Ay 5:9 Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa,
yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.
19 #
2Sam 7:26; Hes 14:21; Za 41:13 Jina lake tukufu lisifiwe milele,
ulimwengu wote ujae utukufu wake.
Amen na Amen.
20 #
Rut 4:17
Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.