73
KITABU CHA TATU
(Zaburi 73–89)
Zaburi 73
Haki Ya Mungu
Zaburi ya Asafu.
1 #
Za 24:4; 5:8 Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,
kwa wale ambao mioyo yao ni safi.
2 #
Kum 32:35; Za 69:2; Efe 4:27 Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza;
nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama.
3 #
Mit 3:31; 23:17; 24:1-2; Ay 9:24; 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15 Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna
nilipoona kufanikiwa kwa waovu.
4Wao hawana taabu,#73:4 Tafsiri nyingine zinasema: hawana maumivu katika kufa kwao.
miili yao ina afya na nguvu.
5 #
Za 73:12; Eze 23:42 Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine,
wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.
6 #
Law 26:19; Mwa 6:11; 41:42; Wim 4:9; Eze 16:11; Mit 4:17; Mhu 8:11 Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao,
wamejivika jeuri.
7 #
Za 7:10
Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi,
majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo.
8 #
Za 10:7; 12:5; 41:5; Eze 25:15; Kol 3:8; 2Pet 2:18; Yud 16 Hudhihaki na kusema kwa ukorofi,
katika majivuno yao wanatishia kutesa.
9 #
Ufu 13:6
Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu,
nazo ndimi zao humiliki duniani.
10Kwa hiyo watu wao huwageukia
na kunywa maji tele.#73:10 Au: na kupokea yote wasemayo.
11 #
Ay 22:13; Za 94:7 Wanasema, “Mungu awezaje kujua?
Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?”
12 #
Za 73:5; 49:6 Hivi ndivyo walivyo waovu:
siku zote hawajali,
wanaongezeka katika utajiri.
13 #
Ay 9:29-31; 21:15; Za 24:4; Mal 3:14; Mwa 44:16; Ebr 10:19-22 Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure,
ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.
14 #
Za 73:5
Mchana kutwa nimetaabika,
nimeadhibiwa kila asubuhi.
15Kama ningesema, “Nitasema hivi,”
ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.
16 #
Mhu 8:17
Nilipojaribu kuelewa haya yote,
yalikuwa magumu kwangu kuelewa.
17 #
Kut 15:17; Ay 8:13; Flp 3:19; Za 15:1; 77:13 Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu,
ndipo nilipotambua mwisho wao.
18 #
Kum 32:35; Za 35:6; 17:13 Hakika unawaweka mahali pa utelezi,
unawaangusha chini kwa uharibifu.
19 #
Kum 28:20; Mit 24:22; Isa 47:11; Mwa 19:15 Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula,
wanatoweshwa kabisa na vitisho!
20 #
Za 78:65; Isa 29:8; Ay 20:8; Mit 12:11; 28:19 Kama ndoto mtu aamkapo,
hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana,
utawatowesha kama ndoto.
21Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa,
na roho yangu ilipotiwa uchungu,
22 #
Za 49:10; 92:6; 49:12, 20; Mhu 3:18; 9:12 nilikuwa mpumbavu na mjinga,
nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.
23 #
Mwa 48:13
Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote,
umenishika mkono wangu wa kuume.
24 #
Za 48:14; 1Fal 22:5; Isa 58:8; Yn 14:3; 2Kor 5:1 Unaniongoza kwa shauri lako,
hatimaye utaniingiza katika utukufu.
25 #
Za 16:2; Flp 3:8 Nani niliye naye mbinguni ila wewe?
Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.
26 #
Kum 32:9; Za 18:1; 84:2; 31:10; 40:12 Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,
bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu
na fungu langu milele.
27 #
Za 34:21; Law 6:2; Yer 5:11; Hos 4:12; 9:1 Wale walio mbali nawe wataangamia,
unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
28 #
Sef 3:2; Yak 4:8; Za 40:5; 26:7; 9:9; Ebr 10:22 Lakini kwangu mimi,
ni vyema kuwa karibu na Mungu.
Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu;
nami nitayasimulia matendo yako yote.