74
Zaburi 74
Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa
Utenzi wa Asafu.
1 #
Yer 23:1; Za 43:2; 44:23; 95:7; 79:13; 100:3; Eze 34:8, 31; Lk 12:32 Ee Mungu, mbona umetukataa milele?
Mbona hasira yako inatoka moshi
juu ya kondoo wa malisho yako?
2 #
1Kor 6:20; Kum 32:7; Kut 34:9; 15:13, 16; Isa 48:20; Za 2:6; 43:3; 68:16; Isa 46:13; Oba 1:17; Yoe 3:17, 21 Kumbuka watu uliowanunua zamani,
kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa:
Mlima Sayuni, ambamo uliishi.
3 #
Isa 44:26; 52:9 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,
uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.
4 #
Mao 2:7; Hes 2:2; Yer 4:6; Dan 6:27 Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,
wanaweka bendera zao kama alama.
5 #
Yer 46:23
Walifanya kama watu wanaotumia mashoka
kukata kichaka cha miti.
6 #
1Fal 6:18
Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa
kwa mashoka na vishoka vyao.
7 #
Law 15:31; 20:3; Mdo 21:28; Za 75:1 Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako.
8 #
2Fal 25:9; Za 83:4; 94:5; Yer 34:22; 52:13; 21:10; 2Nya 36:19 Walisema mioyoni mwao,
“Tutawaponda kabisa!”
Walichoma kila mahali ambapo Mungu
aliabudiwa katika nchi.
9 #
Kut 4:17; 10:1; 1Sam 3:1; Mik 3:6; Mt 16:4 Hatukupewa ishara za miujiza;
hakuna manabii waliobaki,
hakuna yeyote kati yetu ajuaye
hali hii itachukua muda gani.
10 #
Za 6:3; 79:5; 80:4; 74:22; 44:16 Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?
Je, adui watalitukana jina lako milele?
11 #
Kut 15:6; Neh 5:13; Eze 5:3 Kwa nini unazuia mkono wako,
mkono wako wa kuume?
Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako
na uwaangamize!
12 #
Za 2:6; 24:7; 68:24; 44:4 Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani,
unaleta wokovu duniani.
13 #
Isa 51:9; 27:1; Eze 29:3; 32:2; Kut 14:21 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;
ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.
14 #
Hes 14:9; Za 72:9; Ay 3:8; Isa 13:21; 23:13; 34:14; Yer 50:39 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani#74:14 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.
nawe ukamtoa kama chakula
kwa viumbe vya jangwani.
15 #
Kut 14:29; 17:6; Hes 20:11; Isa 11:16; Hab 3:9; Ufu 16:12; Yos 2:10 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito,
ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.
16 #
Mwa 1:16; Za 136:7-9 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,
uliziweka jua na mwezi.
17 #
Mdo 17:26; Kum 32:8; Mwa 8:22 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,
ulifanya kiangazi na masika.
18 #
Ufu 16:19; Kum 32:9 Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki,
jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.
19 #
Mwa 8:8; Isa 59:11; Za 9:18 Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu;
usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.
20 #
Mwa 6:18; 17:7; Law 26:44; Yer 33:21; Ay 34:22 Likumbuke agano lako,
maana mara kwa mara mambo ya jeuri
yamejaa katika sehemu za giza nchini.
21 #
Isa 58:10; Za 9:9, 18; 10:18; 103:6; 35:10 Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu;
maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.
22 #
Za 17:13; 53:1 Inuka, Ee Mungu, ujitetee;
kumbuka jinsi wapumbavu
wanavyokudhihaki mchana kutwa.
23 #
Isa 31:4; Za 65:7; 46:6; Hes 25:17 Usipuuze makelele ya watesi wako,
ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.