75
Zaburi 75
Mungu Ni Mwamuzi
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1 #
Yos 3:5; Za 44:1; 71:16; 77:12; 105:2; 107:8, 15; 145:5, 12, 18 Ee Mungu, tunakushukuru,
tunakushukuru wewe,
kwa kuwa jina lako li karibu;
watu husimulia matendo yako ya ajabu.
2 #
Kut 13:10; Za 7:11 Unasema, “Ninachagua wakati maalum;
ni mimi nihukumuye kwa haki.
3 #
Ebr 1:3; Isa 24:19; 1Sam 2:8; 2Sam 22:8 Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,
ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.
4 #
Za 5:5; Zek 1:21; 1Sam 2:3 Kwa wale wenye majivuno ninasema,
‘Msijisifu tena,’
kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.
5 #
Ay 15:25
Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;
msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”
6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi
au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.
7 #
Mwa 16:5; Ufu 18:8; 1Sam 2:7; Ay 5:11; Za 50:6; 58:11; 147:6; Eze 21:26; Dan 2:21; Lk 1:52 Bali Mungu ndiye ahukumuye:
Humshusha huyu na kumkweza mwingine.
8 #
Mit 23:30; Isa 51:17; Yer 25:15; Zek 12:2; Ufu 14:10; Ay 21:20 Mkononi mwa Bwana kuna kikombe
kilichojaa mvinyo unaotoka povu
uliochanganywa na vikolezo;
huumimina, nao waovu wote wa dunia
hunywa mpaka tone la mwisho.
9 #
Za 40:10; 76:6; 108:1; Mwa 24:12 Bali mimi, nitatangaza hili milele;
nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.
10 #
Za 89:17; 92:10; 112:9; 148:14 Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,
bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.