Zaburi 76
NEN

Zaburi 76

76
Zaburi 76
Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1 # Za 99:3 Katika Yuda, Mungu anajulikana,
jina lake ni kuu katika Israeli.
2 # Mwa 14:18; Ebr 7:1; Za 2:6; 2Sam 5:7 Hema lake liko Salemu,
makao yake katika Sayuni.
3 # Za 46:9; Eze 39:9 Huko alivunja mishale imetametayo,
ngao na panga, silaha za vita.
4 # Za 36:9; Eze 38:12 Wewe unangʼaa kwa mwanga,
mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.
5 # Amu 20:44; Za 13:3; Mt 9:24; Isa 46:12; Yer 51:39 Mashujaa hulala wametekwa nyara,
hulala usingizi wao wa mwisho;
hakuna hata mmoja wa watu wa vita
anayeweza kuinua mikono yake.
6 # Kut 15:1; Zek 12:4; Nah 2:13; Za 50:21 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
farasi na gari la vita vilikaa kimya.
7 # Ay 41:10; Nah 1:6; 1Nya 16:25; Ezr 9:15; Ufu 6:17; Za 2:5 Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa.
Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?
8 # 1Nya 16:30; Eze 38:20 Kutoka mbinguni ulitamka hukumu,
nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:
9 # Za 9:8; 58:11; 74:22; 82:8; 96:13; 72:4 wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu,
kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.
10 # Kut 9:16; Rum 9:17 Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa,
na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi.
11 # Mhu 5:4-5; Za 68:35; Law 22:18; Za 50:14; 2Nya 32:23 Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza;
nchi zote za jirani na walete zawadi
kwa Yule astahiliye kuogopwa.
12Huvunja roho za watawala;
anaogopwa na wafalme wa dunia.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014