Zaburi 78
NEN

Zaburi 78

78
Zaburi 78
Mungu Na Watu Wake
Utenzi wa Asafu.
1 # Kut 19:5; Kum 32:29; Isa 51:4; 55:3 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu,
sikilizeni maneno ya kinywa changu.
2 # Za 49:4; Mt 13:35 Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo,
nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:
3 # Za 44:1; Amu 6:13 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua,
yale ambayo baba zetu walituambia.
4 # Kut 12:26; Yos 4:6, 7; Kum 4:9; 11:19; 32:7; Za 71:18; 26:7; 71:17 Hatutayaficha kwa watoto wao;
tutakiambia kizazi kijacho
matendo yastahiliyo sifa ya Bwana,
uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.
5 # Za 19:7; 81:5; 147:19 Aliagiza amri kwa Yakobo
na akaweka sheria katika Israeli,
ambazo aliwaamuru baba zetu
wawafundishe watoto wao,
6 # Za 22:31; 102:18 ili kizazi kijacho kizijue,
pamoja na watoto ambao watazaliwa,
nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.
7 # Kum 6:12; 5:29 Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu,
nao wasingesahau matendo yake,
bali wangalizishika amri zake.
8 # 2Nya 30:7; Kut 32:9; 23:21; Kum 21:18; Isa 30:9; 65:2 Ili wasifanane na baba zao,
waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi,
ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake,
ambao roho zao hazikumwamini.
9 # Za 78:57; 1Nya 12:2; Hos 7:16; Amu 20:39 Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde,
walikimbia siku ya vita.
10 # Yos 7:10; 2Fal 17:15; Kut 16:28; Yer 11:8 Hawakulishika agano la Mungu
na walikataa kuishi kwa sheria yake.
11 # Za 106:13; Isa 17:10; Yer 2:32 Walisahau aliyokuwa ameyatenda,
maajabu aliyokuwa amewaonyesha.
12 # Neh 9:17; Za 106:22; Kut 11:9; Hes 13:22; Mwa 32:3; Isa 19:11 Alitenda miujiza machoni mwa baba zao,
huko Soani, katika nchi ya Misri.
13 # Kut 14:21, 22; 15:8; Za 66:6; 136:13 Aliigawanya bahari akawapitisha,
alifanya maji yasimame imara kama ukuta.
14 # Kut 13:21; Za 105:39 Aliwaongoza kwa wingu mchana
na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.
15 # Hes 20:11; 1Kor 10:4; Kut 17; 6; Za 105:41; Isa 41:18 Alipasua miamba jangwani
na akawapa maji tele kama bahari,
16 # Kum 9:21 alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka,
akayafanya maji yatiririke kama mito.
17 # Za 78:32 Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake,
wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.
18 # Kut 15:24; 17:2; 1Kor 10:9; Hes 11:4 Kwa makusudi walimjaribu Mungu,
wakidai vyakula walivyovitamani.
19 # Hes 11:4; 21:5 Walinena dhidi ya Mungu, wakisema,
“Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?
20 # Hes 20:11; Kut 17:6 Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu,
vijito vikatiririka maji mengi.
Lakini je, aweza kutupa chakula pia?
Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?”
21 # Hes 11:1 Bwana alipowasikia, alikasirika sana,
moto wake ukawa dhidi ya Yakobo,
na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli,
22 # Kum 1:32; Ebr 3:19; 3:10 kwa kuwa hawakumwamini Mungu,
wala kuutumainia ukombozi wake.
23 # Mwa 7:11; Kum 28:12; 2Fal 7:2 Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu
na kufungua milango ya mbingu,
24 # Kut 16:4; Yn 6:31; Neh 9:15, 20; 1Kor 10:3 akawanyeshea mana ili watu wale;
aliwapa nafaka ya mbinguni.
25Watu walikula mkate wa malaika,
akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula.
26 # Hes 11:31 Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu
na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake.
27 # Kut 16:13; Hes 11:31 Aliwanyeshea nyama kama mavumbi,
ndege warukao kama mchanga wa pwani.
28Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao,
kuzunguka mahema yao yote.
29 # Hes 11:20 Walikula na kusaza,
kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.
30 # Hes 11:33 Kabla hawajamaliza kula walichokitamani,
hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,
31 # Isa 10:16 hasira ya Mungu ikawaka juu yao,
akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao,
akiwaangusha vijana wa Israeli.
32 # Za 78:11, 17, 22 Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi,
licha ya maajabu yake, hawakuamini.
33 # Hes 14:29, 35 Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili
na miaka yao katika vitisho.
34 # Kum 4:29; Hos 5:15; Hes 5:15 Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao,
waliosalia walimtafuta,
walimgeukia tena kwa shauku.
35 # Mwa 49:24; Kum 9:26 Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao,
kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.
36 # Eze 33:31 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,
wakisema uongo kwa ndimi zao,
37 # Za 78:8; Mdo 8:21 mioyo yao haikuwa thabiti kwake,
wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
38 # Kut 34:6; Neh 9:17; Za 25:11; 85:2; 86:15; 1Fal 21:29; Isa 1:25; 27:9; 48:9, 10; 30:18; Mik 7:18; Rum 2:4; Dan 11:35 Hata hivyo alikuwa na huruma,
alisamehe maovu yao
na hakuwaangamiza.
Mara kwa mara alizuia hasira yake,
wala hakuchochea ghadhabu yake yote.
39 # Mwa 6:3; Isa 29:5; Ay 7:7; Yak 4:14; Yn 3:6 Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu,
upepo upitao ambao haurudi.
40 # Kut 23:21; Za 95:8; 106:14; Efe 4:30 Mara ngapi walimwasi jangwani
na kumhuzunisha nyikani!
41 # Kut 17:2; 2Fal 19:22; Za 71:22; 89:18 Walimjaribu Mungu mara kwa mara,
wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
42 # Amu 3:7; Neh 9:17; Za 27:11 Hawakukumbuka uwezo wake,
siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,
43 # Kut 10:1; 3:20 siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri,
maajabu yake huko Soani.
44 # Kut 7:20, 21; Za 105:29; 78:45 Aligeuza mito yao kuwa damu,
hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.
45 # Kut 8:2, 6, 24; Za 105 Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala,
na vyura wakawaharibu.
46 # Nah 3:15; Kut 10:13 Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao,
mazao yao kwa nzige.
47 # Za 105:32; 147:17; Kut 9:23 Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe
na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.
48 # Kut 9:25 Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe,
akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.
49 # Kut 15:7; Mwa 19:13; 1Kor 10:10; Rum 2:8 Aliwafungulia hasira yake kali,
ghadhabu yake, hasira na uadui,
na kundi la malaika wa kuharibu.
50Aliitengenezea njia hasira yake,
hakuwaepusha na kifo,
bali aliwaachia tauni.
51 # Mwa 9:12; Kut 12:12; Za 135:8; 105:23; 106:22 Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri,
matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.
52 # Ay 21:11; Za 28:9; 77:20 Lakini aliwatoa watu wake kama kundi,
akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.
53 # Kut 14:28; 15:7; Za 106:10 Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa,
bali bahari iliwameza adui zao.
54 # Kut 15:17; Za 44:3 Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu,
hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.
55 # Za 44:2; Kum 1:38; Yos 13:7; Mdo 13:19 Aliyafukuza mataifa mbele yao,
na kuwagawia nchi zao kama urithi,
aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.
56Lakini wao walimjaribu Mungu,
na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana,
wala hawakuzishika sheria zake.
57 # 2Nya 30:7; Za 78:9; Eze 20:27; Hos 7:16 Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu,
wakawa wasioweza kutegemewa
kama upinde wenye kasoro.
58 # Amu 2:12; Law 26:30; Kut 20:4; Kum 12:2; 5:8; 32:21; Hes 33:51 Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu,
wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.
59 # Za 55:19; Law 26:28; Hes 32:14; Kum 32:19; Ebr 4:13 Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana,
akamkataa Israeli kabisa.
60 # Yos 18:1; Eze 8:6; 1Sam 4:11; Yer 7:12 Akaiacha hema ya Shilo,
hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.
61 # Amu 18:30; 1Sam 4:12; Za 132:8; 1Sam 4:17 Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani,
utukufu wake mikononi mwa adui.
62 # Kum 28:25; 1Sam 10:1 Aliachia watu wake wauawe kwa upanga,
akaukasirikia sana urithi wake.
63 # 1Fal 4:32; Yer 7:32; 16:9; 25:10; Hes 11:1 Moto uliwaangamiza vijana wao,
na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,
64 # Ay 27:15; 1Sam 4:17 makuhani wao waliuawa kwa upanga,
wala wajane wao hawakuweza kulia.
65 # Za 44:23; Isa 42:13 Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini,
kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.
66 # 1Sam 5:6 Aliwapiga na kuwashinda adui zake,
akawatia katika aibu ya milele.
67 # Yer 7:15; Hos 9:13; 12:1 Ndipo alipozikataa hema za Yosefu,
hakulichagua kabila la Efraimu,
68 # Hes 1:7; Kut 15:17; Za 68:16; 108:8 lakini alilichagua kabila la Yuda,
Mlima Sayuni, ambao aliupenda.
69 # Za 15:1; 1Fal 6:1 Alijenga patakatifu pake kama vilele,
kama dunia ambayo aliimarisha milele.
70 # 1Sam 16:1 Akamchagua Daudi mtumishi wake
na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.
71 # Mwa 37:2; Za 28:9; 2Sam 5:2; 1Nya 11:2; Mik 5:2-4; Zek 11:4 Kutoka kuchunga kondoo alimleta
kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo,
wa Israeli urithi wake.
72 # 1Fal 9:4; Mwa 17:1 Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo,
kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014