79
Zaburi 79
Maombi Kwa Ajili Ya Wokovu Wa Taifa
Zaburi ya Asafu.
1 #
Kut 34:9; Law 20:3; 2Fal 25:9; Neh 4:2; Isa 6:11; Yer 26:18 Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako,
wamelinajisi Hekalu lako takatifu,
wameifanya Yerusalemu kuwa magofu.
2 #
Ufu 19:17-18; Kum 28:26; Yer 7:33 Wametoa maiti za watumishi
kuwa chakula cha ndege wa angani
na nyama ya watakatifu wako
kwa wanyama wa nchi.
3 #
Ufu 11:9; Yer 25:33; 16:4 Wamemwaga damu kama maji
kuzunguka Yerusalemu yote,
wala hakuna yeyote wa kuwazika.
4 #
Eze 5:14; Za 39:8; 44:13 Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu,
cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka.
5 #
Za 74:10; 74:1; 85:5; Kum 29:20; Za 89:46; Sef 3:8; Eze 36:5 Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele?
Wivu wako utawaka kama moto hadi lini?
6 #
Ufu 16:1; Za 2:5; 110:5; 14:4; 53:4; 147:20; 69:24; Yer 10:25; Isa 45:4 Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali,
juu ya falme za hao wasioliitia jina lako,
7 #
Isa 9:12; Yer 10:25 kwa maana wamemrarua Yakobo
na kuharibu nchi ya makao yake.
8 #
Mwa 9:25; Yer 44:21; Za 116:6; 142:6 Usituhesabie dhambi za baba zetu,
huruma yako na itujie hima,
kwa maana tu wahitaji mno.
9 #
2Nya 14:11; 25:11; 31:3; Yer 14:7; Yos 7:9 Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,
kwa ajili ya utukufu wa jina lako;
tuokoe na kutusamehe dhambi zetu
kwa ajili ya jina lako.
10 #
Za 42:3; 94:1; Ufu 6:10; Za 79:3 Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wenu?”
Mbele ya macho yetu,
dhihirisha kati ya mataifa
kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa
ya watumishi wako.
11 #
Hes 14:17
Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako;
kwa nguvu za mkono wako
hifadhi wale waliohukumiwa kufa.
12 #
Isa 65:6; Yer 32:18; Mwa 4:15 Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao
aibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana.
13 #
Za 44:8; 74:1; Isa 43:21 Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako,
tutakusifu milele;
toka kizazi hadi kizazi
tutasimulia sifa zako.