80
Zaburi 80
Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu.
1 #
Kut 25:22; 1Sam 4:4; Za 77:20; 89:1; Kum 33:2 Ee Mchungaji wa Israeli tusikie,
wewe umwongozaye Yosefu kama kundi;
wewe uketiye katika kiti cha enzi
katikati ya makerubi, angaza
2 #
Hes 2:18-24; Za 35:23; 54:1; 71:2; 109:26; 116:4; 119:94 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.
Uamshe nguvu zako,
uje utuokoe.
3 #
Za 71:20; 85:4; Yer 31:18; Mao 5:21; Hes 6:25; Za 80:7, 19; 1Fal 18:37 Ee Mungu, uturejeshe,
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.
4 #
Za 74:10; Kum 29:20 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,
hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi
dhidi ya maombi ya watu wako?
5 #
Ay 3:24; Isa 30:20 Umewalisha kwa mkate wa machozi,
umewafanya wanywe machozi bakuli tele.
6 #
Za 79:4
Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu,
na adui zetu wanatudhihaki.
7 #
Za 80:3
Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
nasi tuweze kuokolewa.
8 #
Isa 5:1-2, 7; Yer 2:21; Mt 21:33-41; Kut 15:17; 23:28-30; Yos 13:6; Mdo 7:45; Eze 15:6 Ulileta mzabibu kutoka Misri,
ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
9Uliandaa shamba kwa ajili yake,
mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
11 #
Kut 23:31; Za 72:8 Matawi yake yalienea mpaka Baharini,#80:11 Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania.
machipukizi yake mpaka kwenye Mto.#80:11 Yaani Mto Frati.
12 #
Isa 5:5; 30:13; Za 89:40; Yer 39:8 Mbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake?
13 #
Yer 5:6
Nguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
14 #
Kum 26:15; Zek 1:12, 16, 17; Isa 63:15 Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!
Tazama chini kutoka mbinguni na uone!
Linda mzabibu huu,
15 #
Isa 49:5
mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,
mwana uliyemlea
kwa ajili yako mwenyewe.
16 #
Za 79:1; Kum 28:20 Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,
unapowakemea, watu wako huangamia.
17 #
Ay 25:6; Za 89:21; 110:1; Kut 4:22; Dan 7:13, 14; Yn 5:21-27 Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume,
mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
18 #
Za 85:6; Isa 57:15; Hos 6:2 Ndipo hatutakuacha tena,
utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.
19 #
Hes 6:25; Za 27:4, 9 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.