81
Zaburi 81
Wimbo Wa Sikukuu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu.
1 #
Za 66:1; 81:4 Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu;
mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!
2 #
Kut 15:20; Za 92:3; Ay 21:12 Anzeni wimbo, pigeni matari,
pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.
3 #
Kut 19:13; Neh 10:33 Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume
wakati wa Mwandamo wa Mwezi,
na wakati wa mwezi mpevu,
katika siku ya Sikukuu yetu;
4 #
Za 81:1; Law 23:24; Hes 10:10 hii ni amri kwa Israeli,
agizo la Mungu wa Yakobo.
5 #
Kut 11:4; Za 114:1 Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu
alipotoka dhidi ya Misri,
huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa.
6 #
Kut 1:14; Isa 9:4; 52:2 Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao;
mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu.
7 #
Kut 2:23; 19:19; 17:7; Kum 33:8 Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa,
nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo;
nilikujaribu katika maji ya Meriba.
8 #
Za 50:7; 78:1 “Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya:
laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!
9 #
Kut 20:3
Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu;
msimsujudie mungu wa kigeni.
10 #
Kut 6:6; 13:3; 29:46; Eze 2:8; Za 107:9; 37:3; Yn 13:7 Mimi ni Bwana Mungu wako,
niliyekutoa nchi ya Misri.
Panua sana kinywa chako
nami nitakijaza.
11 #
Kut 32:1-6
“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza;
Israeli hakutaka kunitii.
12 #
Eze 20:25; Mdo 7:42; Rum 1:24 Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao
wafuate mashauri yao wenyewe.
13 #
Kum 5:29; Isa 48:18; Yer 44:4, 5; Mt 23:37 “Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza,
kama Israeli wangalifuata njia zangu,
14 #
Za 47:3; Amo 1:8 ningaliwatiisha adui zao kwa haraka,
na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!
15 #
2Sam 22:45
Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake,
na adhabu yao ingedumu milele.
16 #
Kum 32:14
Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora,
na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”