82
Zaburi 82
Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki
Zaburi ya Asafu.
1 #
Mhu 5:8; Kut 21:6; Za 7:8; 58:11; Isa 3; 13; 66:16; Yoe 3:12; Ay 21:22 Mungu anaongoza kusanyiko kuu,
anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:
2 #
Kum 1:17; Za 58:1-2; Mit 18:5 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki
na kuonyesha upendeleo kwa waovu?
3 #
Kum 24:17; Za 140:12; Yer 5:28; 22:16 Teteeni wanyonge na yatima,
tunzeni haki za maskini na walioonewa.
4Mwokoeni mnyonge na mhitaji,
wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.
5 #
Za 11:3; 14:4; 53:2; Ay 30:26; Isa 5:30; 8:21-22; 9:2; 59:9; 60:2; Yer 13:16; 23:12, 16; Mao 3:2; Amu 5:4 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote.
Wanatembea gizani;
misingi yote ya dunia imetikisika.
6 #
Kut 22:9; Yn 10:34 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;
ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’
7 #
Za 49:12; Eze 31:14 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;
mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”
8 #
Za 12:5; 76:9; 2:8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,
kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.