83
Zaburi 83
Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli
Wimbo. Zaburi ya Asafu.
1 #
Za 28:1; 35:22; Isa 42:14; 57:11; 62:1; 64:12 Ee Mungu, usinyamaze kimya,
usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.
2 #
Za 2:1; Isa 17:12; Amu 8:28 Tazama watesi wako wanafanya fujo,
jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.
3 #
Kut 1:10; Za 31:13; 17:14 Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako,
wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.
4 #
Es 3:6; Yer 33:24; 11:19; 2Sam 10:6; 2Nya 20:1 Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa,
ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”
5 #
Za 2:2
Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja,
wanafanya muungano dhidi yako,
6 #
Za 137:7; Isa 34:5; Yer 49:7; Amo 1:11; 2Nya 20:1; Mwa 25:16 mahema ya Edomu na Waishmaeli,
ya Wamoabu na Wahagari,
7 #
Yos 13:5; Mwa 19:38; 14:7; Kut 17:14; 15:14; Isa 23:3; Eze 27:3 Gebali,#83:7 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). Amoni na Amaleki,
Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.
8 #
Mwa 10:11; Kum 2:9 Hata Ashuru wameungana nao
kuwapa nguvu wazao wa Loti.
9 #
Hes 31:7, 8; Isa 9:4; Yos 11:1; Amu 4:2, 15, 23, 24; 7:1, 2, 3; Mwa 25:2 Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,
na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini
hapo kijito cha Kishoni,
10 #
1Sam 28:7; 2Fal 9:37; Isa 5:25; Yer 8:2; 9:22; 16:4; 25:33; Sef 1:17 ambao waliangamia huko Endori
na wakawa kama takataka juu ya nchi.
11 #
Amu 7:25; 8:5 Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,
watawala wao kama Zeba na Salmuna,
12 #
2Nya 20:11; Eze 35:10 ambao walisema, “Na tumiliki nchi
ya malisho ya Mungu.”
13 #
Ay 13:25
Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli,
kama makapi yapeperushwayo na upepo.
14 #
Kum 32:22; Isa 9:13 Kama vile moto uteketezavyo msitu
au mwali wa moto unavyounguza milima,
15 #
Za 50:3; Ay 9:17 wafuatilie kwa tufani yako
na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.
16 #
Za 34:5; 109:29; 132:18 Funika nyuso zao kwa aibu
ili watu walitafute jina lako, Ee Bwana.
17 #
2Fal 19:26; Za 35:4 Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele,
na waangamie kwa aibu.
18 #
Za 68:4; 7:8; 18:13 Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako ni Bwana,
kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.