Zaburi 84
NEN

Zaburi 84

84
Zaburi 84
Kuionea Shauku Nyumba Ya Mungu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora.
1 # Kum 33:27; Za 27:4; 43:3; 90:1; 132:5; 26:8; 27:4; Ebr 9:23; Ufu 21:2, 3 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
makao yako yapendeza kama nini!
2 # Ay 19:27; Yos 3:10 Nafsi yangu inatamani sana,
naam, hata kuona shauku,
kwa ajili ya nyua za Bwana;
moyo wangu na mwili wangu
vinamlilia Mungu Aliye Hai.
3 # Za 2:6; 5:2; 43:4; Yer 44:11 Hata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima.
5 # Za 81:1; Yer 31:6 Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
6 # Ay 38:26; Yoe 2:23 Wanapopita katika Bonde la Baka,#84:6 Yaani Bonde la Vilio.
hulifanya mahali pa chemchemi,
pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.#84:6 Au: baraka.
7 # Ay 17:9; Kum 16:16; 1Fal 8:1 Huendelea toka nguvu hadi nguvu,
hadi kila mmoja afikapo
mbele za Mungu huko Sayuni.
8 # Za 4:1 Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu;
nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
9 # 1Sam 16:6; Za 2:2; 59:11; 18:50; 132:17 Ee Mungu, uitazame ngao yetu,
mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
10 # 1Nya 23:5 Siku moja katika nyua zako ni bora
kuliko siku elfu mahali pengine;
afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu
kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
11 # Isa 60:19; Yer 43:13; Ufu 21:23; Mwa 15:1; Za 34:10 Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao,
Bwana hutoa wema na heshima;
hakuna kitu chema anachowanyima
wale ambao hawana hatia.
12 # Za 2:12 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014