85
Zaburi 85
Maombi Kwa Ajili Ya Ustawi Wa Taifa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.
1 #
Kum 30:3; Za 14:7; Yer 30:18; Eze 39:25 Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako.
Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.#85:1 Au: Uliwarudisha mateka wa Yakobo.
2 #
Hes 14:19; Kut 32:30; Za 78:38 Ulisamehe uovu wa watu wako,
na kufunika dhambi zao zote.
3 #
Za 78:38; 106:23; Dan 9:16; Kut 32:12; Yn 3:9; Kum 13:17 Uliweka kando ghadhabu yako yote
na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.
4 #
Za 71:20; 65:5 Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena,
nawe uiondoe chuki yako juu yetu.
5 #
Za 50:21
Je, utatukasirikia milele?
Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?
6 #
Za 80:18; Flp 3:1; Hab 3:2 Je, hutatuhuisha tena,
ili watu wako wakufurahie?
7 #
Za 6:4; 27:1 Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana,
utupe wokovu wako.
8 #
Law 26:6; Isa 60:17; Yn 14:27; 2The 3:16; Mit 26:11; 27:22; Hab 2:1; Zek 9:10; 2Pet 2:20 Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana;
anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake:
lakini nao wasirudie upumbavu.
9 #
Za 27:1; Kut 29:43; Isa 43:3; 45:8; 46:13; 62:11; 51:5; 56:1; 60:19; Hag 2:9; Zek 2:5 Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao,
ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.
10 #
Isa 32:17; Mit 3:3; Lk 2:14; Yn 1:17; 14:27; Za 89:14; 115:1; 72:2, 3; Mik 7:20 Upendo na uaminifu hukutana pamoja,
haki na amani hubusiana.
11 #
Isa 45:8
Uaminifu huchipua kutoka nchi,
haki hutazama chini kutoka mbinguni.
12 #
Za 67:6; 84:11; Yak 1:17; Law 26:4; Zek 8:12 Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema,
nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.
13Haki itatangulia mbele yake
na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.