Zaburi 87
NEN

Zaburi 87

87
Zaburi 87
Sifa Za Yerusalemu
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.
1 # Za 48:1 Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2 # Za 2:6 Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
3 # Za 46:4; Isa 60:1 Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
4 # Ay 9:13; 2Sam 8:1; Za 83:7; 45:12; Yoe 3:4; Isa 19:25 “Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu#87:4 Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri. na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,#87:4 Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.
nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”
5 # Eze 48:35; Mt 16:18 Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
6 # Isa 4:3; Kut 32:32; Yer 3:19; Eze 13:9; Za 22:30; 69:28; Mal 3:16 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
7 # Za 149:3; 36:9 Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014