88
Zaburi 88
Kilio Kwa Ajili Ya Kuomba Msaada
Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi.
1 #
Za 51:14; 3:4; 22:2; Lk 18:7 Ee Bwana, Mungu uniokoaye,
nimelia mbele zako usiku na mchana.
2Maombi yangu yafike mbele zako,
utegee kilio changu sikio lako.
3 #
Ay 33:22; Isa 38:10; Za 6:3; 25:17; 107:18 Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu,
na maisha yangu yanakaribia kaburi.#88:3 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
4 #
Za 31:12; 18:1 Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni,
niko kama mtu asiye na nguvu.
5 #
Za 31:22
Nimetengwa pamoja na wafu,
kama waliochinjwa walalao kaburini,
ambao huwakumbuki tena,
ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.
6 #
Za 30:1; 69:15; Mao 3:55; Yon 2:3 Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana,
katika vina vya giza nene.
7 #
Za 7:11; 42:7 Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu,
umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.
8 #
Ay 3:23; 19:13; Za 31:11; Yer 32:2; 33:1 Umenitenga na rafiki zangu wa karibu
na kunifanya chukizo kwao.
Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;
9 #
Za 38:10; 5:2; 143:6; Ay 11:13 nuru ya macho yangu
imefifia kwa ajili ya huzuni.
Ee Bwana, ninakuita kila siku,
ninakunyooshea wewe mikono yangu.
10 #
Za 6:5
Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako?
Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?
11 #
Za 30:9
Je, upendo wako hutangazwa kaburini,
uaminifu wako katika Uharibifu?#88:11 Yaani Abadon.
12 #
Ay 10:21; 31:12; Mhu 8:10 Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza,
au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?
13 #
Za 30:2; 5:3; 55:17; 119:147 Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie;
asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
14 #
Za 43:2; 13:1 Ee Bwana, kwa nini unanikataa
na kunificha uso wako?
15 #
Dan 9:26; Za 9:12; 129:1; Yer 22:21; Eze 16:22; Hos 2:15; Isa 53:8; Ay 6:4; 18:11; 2Kor 4:8 Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo;
nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.
16 #
Za 7:11; Ay 6:4 Ghadhabu yako imepita juu yangu;
hofu zako zimeniangamiza.
17 #
Za 124:4
Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko;
zimenimeza kabisa.
18 #
Za 88:8; 38:11; Ay 19:13 Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu;
giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.