89
Zaburi 89
Wimbo Wakati Wa Taabu Ya Kitaifa
Utenzi wa Ethani Mwezrahi.
1 #
Za 59:16; 36:5; 40:10 Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele;
kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako
ujulikane kwa vizazi vyote.
2 #
Za 36:5
Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele
na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.
3 #
Eze 34:23; Hes 3:5; Ebr 7:21; Mdo 2:30 Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu,
nimemwapia mtumishi wangu Daudi,
4 #
2Sam 7:12-16; Lk 1:32, 33; Mt 1:1; Isa 9:6, 7; Rum 1:3; 1Fal 9:5; 8:16; Eze 37:24, 25; Za 132:11, 12 ‘Nitaimarisha uzao wako milele
na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”
5 #
Za 19:1; 1:5 Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako,
uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.
6 #
Mwa 1:26; Kut 9:14; Za 18:31; 113:5 Kwa kuwa ni nani katika mbingu
anayeweza kulinganishwa na Bwana?
Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni
aliye kama Bwana?
7 #
Ay 5:1; Za 11:1; 47:2 Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana,
anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.
8 #
Isa 6:3; Za 71:19 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,
ni nani aliye kama wewe?
Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu,
na uaminifu wako unakuzunguka.
9 #
Za 65:7; Ay 38:11; Nah 1:4; Mt 8:26 Wewe unatawala bahari yenye msukosuko;
wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.
10 #
Ay 9:13; Za 59:11; 68:1; 92:9; Isa 30:9 Wewe ulimponda Rahabu#89:10 Rahabu hapa ina maana jina la Misri kwa fumbo, yaani mwenye majivuno (lakini sio Rahabu wa Yos 2).
kama mmojawapo wa waliochinjwa;
kwa mkono wako wenye nguvu,
uliwatawanya adui zako.
11 #
Kum 10:14; Za 24:1; 115:6; 1Nya 29:11; Mwa 1:1 Mbingu ni zako, nayo nchi pia ni yako,
uliuwekea ulimwengu msingi
pamoja na vyote vilivyomo.
12 #
Yos 19:22; Kum 3:8; 4:48; Za 98:8; Yos 12:1; Amu 4:6 Uliumba kaskazini na kusini;
Tabori na Hermoni wanaliimbia jina lako kwa furaha.
13 #
Yos 4:24
Mkono wako umejaa uwezo;
mkono wako una nguvu,
mkono wako wa kuume umetukuzwa.
14 #
Za 97:2; 85:10, 11 Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako cha enzi;
upendo na uaminifu vinakutangulia.
15 #
Za 1:1; 44:3; Hes 10:10 Heri ni wale ambao wamejifunza kukusifu kwa shangwe,
wanaotembea katika mwanga
wa uwepo wako, Ee Bwana.
16 #
Za 30:4; 105:3 Wanashangilia katika jina lako mchana kutwa,
wanafurahi katika haki yako.
17 #
Za 18:1, 24; 75:10; 92:10; 112:9; 148:14 Kwa kuwa wewe ni utukufu na nguvu yao,
kwa wema wako unatukuza pembe#89:17 Pembe inawakilisha nguvu. yetu.
18 #
Hos 13:10; Za 18:2; 47:9; Isa 16:5; 33:17, 22 Naam, ngao yetu ni mali ya Bwana,
na mfalme wetu mali ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
19Ulizungumza wakati fulani katika maono,
kwa watu wako waaminifu, ukasema:
“Nimeweka nguvu kwa shujaa,
nimemwinua kijana miongoni mwa watu.
20 #
Mdo 13:22; Za 78:70; Kut 29:7; 1Fal 1:39; 1Sam 2:35; 2Sam 22:51 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,
na nimemtia mafuta yangu matakatifu.
21 #
Za 89:13; 18:35 Kitanga changu kitamtegemeza,
hakika mkono wangu utamtia nguvu.
22 #
Amu 3:15; 2Sam 7:10 Hakuna adui atakayemtoza ushuru,
hakuna mtu mwovu atakayemwonea.
23 #
Za 18:40; 2Sam 7:9 Nitawaponda adui zake mbele zake
na kuwaangamiza watesi wake.
24 #
2Sam 7:15; Za 61:7 Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye,
kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa.
25 #
Za 72:8
Nitauweka mkono wake juu ya bahari,
mkono wake wa kuume juu ya mito.
26 #
Za 62:2; Yer 3:4; 2Sam 7:14; 22:47; 1Nya 22:10; Yn 5:17; Ebr 1:5 Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu,
Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’
27 #
Kol 1:18; Hes 24:7; Za 2:6, 7; Ufu 1:5; 19:16 Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza,
aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia.
28 #
Za 89:33-34; Isa 55:3 Nitadumisha upendo wangu kwake milele,
na agano langu naye litakuwa imara.
29 #
Isa 9:7; Yer 33:17; Dan 7:14; Kum 11:21; Za 89:4, 36 Nitaudumisha uzao wake milele,
kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.
30 #
2Sam 7:14; Yer 9:13 “Kama wanae wataacha amri yangu
na wasifuate sheria zangu,
31kama wakihalifu maagizo yangu
na kutoshika amri zangu,
32 #
2Sam 7:14
nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,
uovu wao kwa kuwapiga,
33 #
2Sam 7:15
lakini sitauondoa upendo wangu kwake,
wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
34 #
Hes 23:19
Mimi sitavunja agano langu
wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
35 #
Za 110:4; Ebr 6:13, 17; Amo 4:2; 8:7 Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu,
nami sitamdanganya Daudi:
36 #
Za 89:4; 2Sam 7:18; Lk 1:33; Yn 12:34 kwamba uzao wake utaendelea milele,
na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
37 #
Yer 31:35; 33:20, 21 kitaimarishwa milele kama mwezi,
shahidi mwaminifu angani.”
38 #
1Nya 28:9; Isa 22:5; Mao 2:2 Lakini wewe umemkataa, umemdharau,
umemkasirikia sana mpakwa mafuta wako.
39 #
Mao 5:16
Umelikana agano lako na mtumishi wako,
na umeinajisi taji yake mavumbini.
40 #
Za 80:12; Isa 22:5; Mao 2:2 Umebomoa kuta zake zote,
na ngome zake zote umezifanya kuwa magofu.
41 #
Amu 2:14; Za 44:13 Wote wapitao karibu wamemnyangʼanya mali zake;
amekuwa dharau kwa jirani zake.
42 #
Za 13:2; 80:6 Umeutukuza mkono wa kuume wa adui zake,
umewafanya watesi wake wote washangilie.
43 #
Za 44:10
Umegeuza makali ya upanga wake,
na hukumpa msaada katika vita.
44Umeikomesha fahari yake,
na kukiangusha kiti chake cha enzi.
45 #
Za 39:5; 44:15; 109:29 Umezifupisha siku za ujana wake,
umemfunika kwa vazi la aibu.
46 #
Za 79:5
Hata lini, Ee Bwana? Utajificha milele?
Ghadhabu yako itawaka kama moto hata lini?
47 #
Mwa 47:9; Ay 7:7; Za 39:5; 1Pet 1:24 Kumbuka jinsi maisha yangu yanavyopita haraka.
Ni kwa ubatili kiasi gani umemuumba mwanadamu!
48 #
Mwa 5:24; Za 22:29; Ebr 11:5 Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,
au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?#89:48 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
49 #
2Sam 7:12; Isa 55:13 Ee Bwana, uko wapi upendo wako mkuu wa mwanzoni,
ambao katika uaminifu wako ulimwapia Daudi?
50 #
Za 69:19
Bwana kumbuka jinsi mtumishi wako amesimangwa,
jinsi ninavyovumilia moyoni mwangu dhihaka za mataifa yote,
51 #
Za 74:10
dhihaka ambazo kwazo adui zako
wamenisimanga, Ee Bwana,
ambazo kwazo wamesimanga
kila hatua ya mpakwa mafuta wako.
52 #
Za 41:13; 72:19 Msifuni Bwana milele!
Amen na Amen.