90
KITABU CHA NNE
(Zaburi 90–106)
Zaburi 90
Umilele Wa Mungu Na Udhaifu Wa Mwanadamu
Maombi ya Mose, mtu wa Mungu.
1 #
Kum 33:27; Efe 2:22; Ufu 21:3 Bwana, wewe umekuwa makao yetu
katika vizazi vyote.
2 #
Ay 38:4, 5; 10:5; 15:7; Mwa 21:33; Isa 9:6; 57:15; Za 102:24-27; Mit 8:23-26 Kabla ya kuzaliwa milima
au hujaumba dunia na ulimwengu,
wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
3 #
Mwa 2:7; 3:9; Ay 7:21; 34:15; 1Kor 15:47; Mhu 12:7 Huwarudisha watu mavumbini,
ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”
4 #
Ebr 13:8; 2Pet 3:8; Ay 10:5 Kwa maana kwako miaka elfu
ni kama siku moja iliyokwisha pita,
au kama kesha la usiku.
5 #
Mwa 19:15; Isa 40:6 Unawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo,
nao ni kama majani machanga ya asubuhi:
6 #
Isa 40:6-8; Ay 14:2; Za 92:7 ingawa asubuhi yanachipua,
ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka.
7Tumeangamizwa kwa hasira yako
na tumetishwa kwa ghadhabu yako.
8 #
2Kor 4:2; Efe 5:12; Ebr 4:13; 4:12, 13; Za 19:12; 50:21; Yer 16:17; Mit 5:21; Mhu 12:14; Rum 2:16; 1Kor 4:5 Umeyaweka maovu yetu mbele yako,
dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako.
9 #
Za 78:33
Tumeishi siku zetu zote chini ya ghadhabu yako,
tunamaliza miaka yetu kwa kuomboleza.
10 #
Isa 23:15, 17; 2Sam 19:35; Ay 5:7; 20:8; 34:15; Yer 25:11 Siku zetu za kuishi ni miaka sabini,
au miaka themanini ikiwa tuna nguvu,
lakini yote ni ya shida na taabu,
nazo zapita haraka, nasi twatoweka.
11 #
Za 7:11; 76:7 Ni nani ajuaye nguvu za hasira yako?
Kwa maana ghadhabu yako ni kubwa
kama hofu tunayopaswa kuwa nayo kwako.
12 #
Za 39:4; 139:16; Mit 16:9; 20:24; Kum 32:29 Tufundishe kuzihesabu siku zetu vizuri,
ili tujipatie moyo wa hekima.
13 #
Za 6:3; Kum 32:36 Ee Bwana, uwe na huruma! Utakawia hata lini?
Wahurumie watumishi wako.
14 #
Za 103:5; 107:9; 145:16, 19; 31:7; 77:8; 143:8 Tushibishe asubuhi kwa upendo wako usiokoma,
ili tuweze kuimba kwa shangwe na kufurahi siku zetu zote.
15Utufurahishe kulingana na siku ulizotuadhibu,
kulingana na miaka tuliyotaabika.
16 #
Za 44:1; Hab 3:2 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,
utukufu wako kwa watoto wao.
17 #
Isa 26:12; 2The 2:16, 17 Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu;
uzithibitishe kazi za mikono yetu:
naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu.