92
Zaburi 92
Wimbo Wa Kumsifu Mungu
Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.
1 #
Za 27:6; 147:1; 135:3 Ni vyema kumshukuru Bwana
na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,
2 #
Za 55:17
kuutangaza upendo wako asubuhi,
na uaminifu wako wakati wa usiku,
3 #
Za 71:22; 1Sam 10:5; Neh 12:27; Za 33:2; 81:2 kwa zeze yenye nyuzi kumi
na kwa sauti ya kinubi.
4 #
Za 5:11; 27:6; 8:6; 111:7; 143:5 Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,
nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.
5 #
Ay 36:24; Ufu 15:3; Za 40:5; 139:17; Isa 28:29; 31:2; Rum 11:33 Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako,
tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!
6 #
Za 73:22
Mjinga hafahamu,
mpumbavu haelewi,
7 #
Ay 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15; Za 37:1 ingawa waovu huchipua kama majani
na wote watendao mabaya wanastawi,
wataangamizwa milele.
8Bali wewe, Ee Bwana,
utatukuzwa milele.
9 #
Za 45:5; 68:1; 89:10 Ee Bwana, hakika adui zako,
hakika adui zako wataangamia.
Wote watendao mabaya watatawanyika.
10 #
Za 89:17; 29:6; 89:10 Umeitukuza pembe#92:10 Pembe inawakilisha nguvu. yangu kama ile ya nyati dume,
mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.
11 #
Za 54:7; 91:8 Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa,
masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.
12 #
Za 72:7; 1:3; 52:8; Yer 17:8; Hos 14:6; Wim 7:7 Wenye haki watastawi kama mtende,
watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,
13 #
Isa 60:21; Mt 15:13; Yn 15:2, 5; Za 135:2 waliopandwa katika nyumba ya Bwana,
watastawi katika nyua za Mungu wetu.
14 #
Za 1:3; Yn 15:2 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,
watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,
15 #
Ay 34:10
wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu;
yeye ni Mwamba wangu,
na ndani yake hamna uovu.”