Zaburi 93
NEN

Zaburi 93

93
Zaburi 93
Mungu Mfalme
1 # 1Nya 16:30, 31; Za 21:5; 65:6; 24:2; 78:69; 97:1; 119:90; 104:1; 96:10; Ay 40:10; Ufu 19:6; Isa 52:7; 59:17 Bwana anatawala, amejivika utukufu;
Bwana amejivika utukufu
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa.
2 # Mit 8:22; 2Sam 7:16; Mwa 21:33 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwako tangu milele.
3 # Isa 17:12, 13; 5:30; Yer 6:23; Za 96:11; 98:7; 107:25, 29; 46:3; Ay 9:8; Isa 51:15; Yer 31:35; Hab 3:10 Bahari zimeinua, Ee Bwana,
bahari zimeinua sauti zake;
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.
4 # Za 29:10; 65:7; Yer 6:23; 18:4; Yon 1:15; Neh 9:32; Ay 9:4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Bwana aishiye juu sana ni mkuu.
5 # Za 29:2; 5:7; 23:6 Ee Bwana, sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014