94
Zaburi 94
Mungu Mlipiza Kisasi Kwa Ajili Ya Wenye Haki
1 #
Mwa 4:24; Za 80:1; Rum 12:19; Kum 33:2 Ee Bwana, ulipizaye kisasi,
Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa.
2 #
Mwa 18:25; Yak 5:9; Hes 10:35; Za 31:23 Ee Mhukumu wa dunia, inuka,
uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili.
3 #
Za 13:2; Mwa 20:3 Hata lini, waovu, Ee Bwana,
hata lini waovu watashangilia?
4 #
Yer 43:2; Za 52:1; Yud 15 Wanamimina maneno ya kiburi,
watenda mabaya wote wamejaa majivuno.
5 #
Za 28:9; 44:2; 74:8; Isa 3:15; Yer 8:21 Ee Bwana, wanawaponda watu wako,
wanawaonea urithi wako.
6 #
Kum 10:18; 20:19; Isa 1:17 Wanamchinja mjane na mgeni,
na kuwaua yatima.
7 #
Ay 22:14; Mwa 24:12 Nao husema, “Bwana haoni,
Mungu wa Yakobo hafahamu.”
8 #
Kum 32:6; Za 73:22 Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu;
enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima?
9 #
Kut 4:11; Mit 20:12 Je, aliyeweka sikio asisikie?
Aliyeumba jicho asione?
10 #
Za 39:11; Ay 35:11; Yn 6:45; Isa 2:3; 28:26; Kut 35:34 Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu?
Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa?
11 #
Za 139:2; Mt 15:26; 9:4; 1Kor 3:20; 1:21 Bwana anajua mawazo ya mwanadamu;
anajua kwamba ni ubatili.
12 #
Ay 5:17; Kum 8:3; 1Kor 11:32; Mit 3:11; Ebr 12:5; 1Sam 12:23 Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe,
mtu unayemfundisha kwa sheria yako,
13 #
Za 86:7; 7:15; 55:23 unampa utulivu siku za shida,
mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa
kwa ajili ya mwovu.
14 #
Kum 31:6; Za 37:28; Rum 11:2; 1Sam 12:22; 1Fal 6:13; Yer 31:37 Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake,
hatauacha urithi wake.
15 #
Za 97:2; 7:10; 11:2; 36:10 Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki,
wote walio na mioyo minyofu wataifuata.
16 #
Hes 10:35; Isa 14:22; Za 17:13; 59:2 Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu?
Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu?
17 #
Za 124:2; 31:17 Kama Bwana asingelinisaidia upesi,
ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.
18 #
Kum 32:35; Ay 12:5 Niliposema, “Mguu wangu unateleza,”
Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.
19 #
Mhu 11:10; Ay 6:10 Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,
faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.
20 #
Za 58:2; Isa 10:1; 2Kor 6:14; Amo 6:3; Yer 22:30; 36:30 Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe,
ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?
21 #
Za 56:6; 106:38; Mit 17:15, 26; 28:21; Isa 5:20, 23; Mt 27:1, 4; Mwa 18:23; Mit 17:15; Kut 23:7 Huungana kuwashambulia wenye haki,
kuwahukumu kufa wasio na hatia.
22 #
Za 18:2; 61:2; 2Sam 22:3 Lakini Bwana amekuwa ngome yangu,
na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia.
23 #
Za 37:38; 145:20; 54:5; 9:5; Mit 2:22; Kut 32:34 Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao
na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao;
Bwana Mungu wetu atawaangamiza.