96
Zaburi 96
Mungu Mfalme Mkuu
(1 Nyakati 16:23-33)
1 #
Za 30:4; 33:3; 40:4; 98:1; 144:9; Isa 42:10; Ufu 5:9 Mwimbieni Bwana wimbo mpya;
mwimbieni Bwana dunia yote.
2 #
Isa 42:10; Ufu 5:9; Za 68:4; 27:1; 71:15 Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake;
tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
3 #
Za 8:1; 71:17; 15:3 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,
matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
4 #
Za 48:1; 89:7; 95:3; Kum 28:58; 1Nya 16:25 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;
yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
5 #
Mwa 1:1; Isa 42:5; 41:24; Law 19:4; Yer 10:11; 2Nya 2:12; Hab 2:18-20; Mdo 19:26; 1Kor 8:4, 5 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,
lakini Bwana aliziumba mbingu.
6 #
Za 21:5; 29:1; 89:17 Fahari na enzi viko mbele yake;
nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
7 #
Za 29:1; 22:27 Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu.
8 #
Za 45:12; 51:19; 72:10; 65:4; 84:10; 92:13; 100:4 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;
leteni sadaka na mje katika nyua zake.
9 #
Kut 15:14; 23:25; Yon 1:9; Za 93:5; 114:7; 33:8 Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake;
dunia yote na itetemeke mbele zake.
10 #
Za 97:1; 24:2; 78:69; 119:90; 93:1; 58:11; 67:4; 98:9 Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.”
Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa;
atawahukumu watu kwa uadilifu.
11 #
Ufu 12:12; Za 97:1; Isa 49:13 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;
bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
12 #
Isa 44:23; 55:12; Eze 17:24; Za 65:13 mashamba na yashangilie,
pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.
Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;
13 #
Ufu 19:11; Za 7:11; Mdo 17:31; Za 86:11 itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja,
anakuja kuihukumu dunia.
Ataihukumu dunia kwa haki,
na mataifa katika kweli yake.