99
Zaburi 99
Mungu Mfalme Mkuu
1 #
1Nya 16:30, 31; Za 97:1; 2Sam 6:2; Kut 15:14; 25:22 Bwana anatawala,
mataifa na yatetemeke;
anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,
dunia na itikisike.
2 #
Za 48:1; 148:13; 2:6; 46:10; 97:9; 113:4; Kut 15:1 Bwana ni mkuu katika Sayuni;
ametukuzwa juu ya mataifa yote.
3 #
Za 103:1; 33:21; 97:12; 76:1; 30:4; 106:47; 111:9; 145:21; 148:5; Kut 15:11 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:
yeye ni mtakatifu!
4 #
1Fal 10:9; Za 98:9; Mwa 18:19, 25; Ufu 15:3; Ay 36:5; Kum 32:3, 4; Isa 11:3-5; Yer 23:5; Za 2:6 Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,
wewe umethibitisha adili;
katika Yakobo umefanya
yaliyo haki na sawa.
5 #
Isa 66:1; Kut 15:2; 1Nya 28:2; Za 132:7 Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,
na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;
yeye ni mtakatifu.
6 #
Kut 24:6; 28:1; 1Sam 7:5; Za 4:3; 91:15 Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,
Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;
walimwita Bwana,
naye aliwajibu.
7 #
Kut 13:21; 19:9; Hes 11:25; 12:5 Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;
walizishika sheria zake na amri alizowapa.
8 #
Hes 14:20; Sef 3:7; Kum 9:20; Kut 22:27; Law 26:18 Ee Bwana, wetu,
ndiwe uliyewajibu,
kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,
ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.
9Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,
mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,
kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.