Wimbo 3
NEN

Wimbo 3

3
1 # Isa 26:9; Wim 5:6 Usiku kucha kwenye kitanda changu
nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye;
nilimtafuta, lakini sikumpata.
2Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,
katika barabara zake na viwanja;
nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.
Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.
3 # Wim 5:7; Isa 21:6-11 Walinzi walinikuta
walipokuwa wakizunguka mji.
Nikawauliza, “Je, mmemwona
yule moyo wangu umpendaye?”
4 # Wim 8:2; 6:9; 8:5; Rum 8:35-39; Mit 8:17; 4:13 Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita
nilimpata yule moyo wangu umpendaye.
Nilimshika na sikumwachia aende
mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu,
katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.
5 # Wim 2:7; 8:4 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza
kwa paa na kwa ayala wa shambani:
Msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe.
Shairi La Tatu
Mpenzi
6 # Wim 8:6; 4:6, 14; Kut 30:34; Yer 2:2 Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani
kama nguzo ya moshi,
anayenukia manemane na uvumba
iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote
vya mfanyabiashara?
7 # 1Sam 8:11 Tazama! Ni gari la Solomoni
lisindikizwalo na mashujaa sitini,
walio wakuu sana wa Israeli,
8 # Ay 15:22; Za 91:5 wote wamevaa panga,
wote wazoefu katika vita,
kila mmoja na upanga wake pajani,
wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.
9Mfalme Solomoni alijitengenezea gari;
alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.
10 # Mt 22:37; Efe 3:19; Rum 5:8 Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha,
kitako chake kwa dhahabu.
Kiti chake kilipambwa kwa zambarau,
gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo
na binti za Yerusalemu.
11 # Isa 3:16; 54:5; 32:9-13; 62:5; Yer 3:14 Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni,
mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji,
taji ambalo mama yake alimvika
siku ya arusi yake,
siku ambayo moyo wake ulishangilia.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014