10
Bwana Ataitunza Yuda
1 #
Law 26:4; 1Fal 8:36; Za 104:13; 135:7; Ay 14:9; Yer 14:22; Yoe 2:32 Mwombeni Bwana mvua wakati wa vuli;
ndiye Bwana atengenezaye mawingu ya tufani.
Huwapa watu manyunyu ya mvua,
pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.
2 #
Eze 21:21; Isa 44:25; 40:19; Yer 23:16; Hes 27:17; Hos 3:4; Mt 9:36 Sanamu huzungumza udanganyifu,
waaguzi huona maono ya uongo;
husimulia ndoto ambazo si za kweli,
wanatoa faraja batili.
Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo
walioonewa kwa kukosa mchungaji.
3 #
Isa 14:9; Yer 25:34; Eze 34:8-10; Kut 4:31; Rut 1:6; Sef 2:7; Lk 1:68; 1Pet 2:12 “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,
nami nitawaadhibu viongozi;
kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote
atalichunga kundi lake,
nyumba ya Yuda,
naye atawafanya kuwa kama farasi
mwenye kiburi akiwa vitani.
4 #
Za 118:22; Mdo 4:11; Isa 22:23; Zek 9:10 Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,
kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,
kutoka kwake utatoka upinde wa vita,
kutoka kwake atatoka kila mtawala.
5 #
2Sam 22:43; Mik 7:10; 5:8; Amo 2:15; Hag 2:22; Zek 12:4 Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa
wanaokanyaga barabara za matope
wakati wa vita.
Kwa sababu Bwana yu pamoja nao,
watapigana na kuwashinda wapanda farasi.
6 #
Eze 30:24; 36:37; Za 102:13; 34:17; Isa 37:19; 14:1; 58:9; 65:24; Zek 8:7-8; 13:9 “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda
na kuiokoa nyumba ya Yosefu.
Nitawarejesha kwa sababu
nina huruma juu yao.
Watakuwa kama watu ambao
sijawahi kuwakataa
kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wao,
nami nitawajibu.
7 #
Zek 9:15; 1Sam 2:1; Isa 60:5; Yoe 2:23 Waefraimu watakuwa kama mashujaa,
mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.
Watoto wao wataona na kufurahi,
mioyo yao itashangilia katika Bwana.
8 #
Isa 5:26; Yer 33:22; Eze 36:11 Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.
Hakika nitawakomboa,
nao watakuwa wengi
kama walivyokuwa mwanzoni.
9 #
Isa 44:21; Eze 6:9 Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,
hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali
watanikumbuka mimi.
Wao na watoto wao watanusurika katika hatari
nao watarudi.
10 #
Isa 11:11; 49:19; Zek 8:8; Yer 50:19; Rum 11:25; Kut 14:26-27 Nitawarudisha kutoka Misri
na kuwakusanya toka Ashuru.
Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,
na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.
11 #
Isa 19:5-7; 51:10; Sef 2:13; Eze 29:15; 30:13 Watapita katika bahari ya mateso;
bahari iliyochafuka itatulizwa
na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka.
Kiburi cha Ashuru kitashushwa,
nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.
12 #
Eze 30:24; Mik 4:5 Nitawaimarisha katika Bwana,
na katika jina lake watatembea,”
asema Bwana.