Zab 101
SUV

Zab 101

101
Ahadi ya Mfalme juu ya Uaminifu na Haki
Ya Daudi. Zaburi.
1Rehema na hukumu nitaziimba,
Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.
2 # 1 Sam 18:14; Mwa 18:19; Kum 6:7; 1 Fal 9:4 Nitaiangalia njia ya unyofu;
Utakuja kwangu lini?
Nitakwenda kwa unyofu wa moyo
Ndani ya nyumba yangu.
3 # Yos 23:6; 1 Sam 12:20 Sitaweka mbele ya macho yangu
Neno la uovu.
Kazi yao waliopotoka naichukia,
Haitaambatana nami.
4 # Mt 7:23; 1 Kor 5:11; 2 Tim 2:19 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,
Lililo ovu sitalijua.
5 # Mit 6:17; Lk 18:14 Amsingiziaye jirani yake kwa siri,
Huyo nitamharibu.
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,
Huyo sitavumilia naye.
6 # Rum 13:4 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
Hao wakae nami.
Yeye aendaye katika njia kamilifu,
Ndiye atakayenitumikia.
7Hatakaa ndani ya nyumba yangu
Mtu atendaye hila.
Asemaye uongo hatathibitika
Mbele ya macho yangu.
8 # Yer 21:12; Hos 9:3 Asubuhi hata asubuhi nitawaharibu
Wabaya wote wa nchi.
Niwatenge wote watendao uovu
Na mji wa BWANA.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia