Zab 112
SUV

Zab 112

112
Baraka za Mwenye Haki
1Haleluya.
Heri mtu yule amchaye BWANA,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
2Wazao wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
3 # Mit 3:16; 15:6; Isa 33:6; Mt 6:33; 2 Kor 6:10 Nyumbani mwake mna utajiri na mali,
Na haki yake yakaa milele.
4Nuru huwazukia wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
5 # Lk 6:35 Heri atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye mambo yake kwa haki.
6Kwa maana hataondoshwa kamwe;
Mwenye haki atakumbukwa milele.
7Hataogopa habari mbaya;
Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.
8Moyo wake umethibitika hataogopa,
Hata awaone watesi wake wameshindwa.
9 # Lk 11:41; Rum 12:13; Mdo 4:35; 20:35; 2 Kor 8:9; 9:9; 1 Tim 6:18 Amekirimu, na kuwapa maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
10 # Lk 13:28 Asiye haki ataona na kusikitika,
Atasaga meno yake na kuyeyuka,
Tamaa ya wasio haki itapotea.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia