Zab 129
SUV

Zab 129

129
Sala ya Kushindwa kwa Adui za Israeli
Wimbo wa Kupanda Mlima
1 # Eze 23:3; Hos 2:15 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Israeli na aseme sasa,
2Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Lakini hawakuniweza.
3 # Ebr 11:36 Wakulima wamelima mgongoni mwangu,
Wamefanya mirefu mifuo yao.
4 # 2 The 1:6 BWANA ndiye mwenye haki,
Amezikata kamba zao wasio haki.
5Na waaibishwe, warudishwe nyuma,
Wote wanaoichukia Sayuni.
6 # Zab 37:2; Yer 17:5-6 Na wawe kama majani ya darini
Yanyaukayo kabla hayajamea.
7Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,
Wala mfunga miganda kifua chake.
8 # Rut 2:4; Zab 118:26 Wala hawasemi wapitao, Amani ya BWANA ikae nanyi,
Twawabariki kwa jina la BWANA.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia