146
Sifa kwa Kupata Msaada wa Mungu
1Haleluya.#146:1Haleluya maana yake ni, Msifuni BWANA.
Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.
2Nitamsifu BWANA muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
3 #
Isa 2:22
Msiwatumainie wakuu,
Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4 #
Mhu 12:7; 1 Kor 2:6 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,
Siku hiyo mawazo yake yapotea.
5 #
Yer 17:7
Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,
6 #
Mik 7:20; Mdo 4:24; 14:15; Ufu 14:7 Aliyezifanya mbingu na nchi,
Bahari na vitu vyote vilivyomo.
Huishika kweli milele,
7Huwafanyia hukumu walioonewa,
Huwapa wenye njaa chakula;
BWANA hufungua waliofungwa;
8BWANA huwafumbua macho waliopofuka;
BWANA huwainua walioinama;
BWANA huwapenda wenye haki;
9BWANA huwahifadhi wageni;
Huwategemeza yatima na mjane;
Bali njia ya wasio haki huipotosha.
10BWANA atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi.
Haleluya.