20
Sala ya Ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Isa 50:10
BWANA akujibu siku ya dhiki,
Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2Akupelekee msaada toka patakatifu pake,
Na kukutegemeza toka Sayuni.
3Azikumbuke sadaka zako zote,
Na kuzitakabali dhabihu zako.
4 #
1 Yoh 5:14,15 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,
Na kuyatimiza mashauri yako yote.
5 #
Isa 12:1,2; 1 Sam 17:45 Na tuushangilie wokovu wako,
Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.
BWANA akutimizie matakwa yako yote.
6Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi#20:6 Au, mtiwa mafuta. wake;
Atamjibu toka mbingu zake takatifu,
Kwa matendo makuu ya wokovu
Ya mkono wake wa kuume.
7 #
Amu 7:7
Hawa wanataja magari na hawa farasi,
Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
8Wao wameinama na kuanguka,
Bali sisi tumeinuka na kusimama.
9BWANA, umwokoe mfalme,
Utuitikie siku tuitayo.