3
Mwamini Mungu katika Dhiki
Zaburi ya Daudi alipomkimbia mwanawe, Absalomu.
1 #
2 Sam 15:13—17:22
BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,
Ni wengi wanaonishambulia,
2 #
2 Sam 16:8; Zab 22:7,8 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,
Hana wokovu huyu kwa Mungu.
3 #
2 Fal 25:27; Zab 27:6 Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,
Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.
4Kwa sauti yangu namwita BWANA
Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.
5 #
Zab 4:8; Mit 3:24; Mdo 12:6 Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka,
Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
6Sitayaogopa makumi elfu ya watu,
Waliojipanga juu yangu pande zote.
7BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,
Maana umewapiga taya adui zangu wote;
Umewavunja meno wasio haki.
8 #
Zab 37:39,40; Mit 21:31; Hes 13:4 Wokovu una BWANA;
Baraka yako na iwe juu ya watu wako.