Zab 4
SUV

Zab 4

4
Ombi la Kuokolewa kutoka kwa Adui
Kwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;
Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;
Unifadhili na kuisikia sala yangu.
2Enyi wanadamu, hata lini utukufu wangu utafedheheka?
Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo?
3 # Kut 33:16; 2 Pet 2:9 Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa;
BWANA atasikia nimwitapo.
4 # Efe 4:26; Mit 3:7 Mwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
5 # Kum 33:19; Zab 37:3 Toeni dhabihu za haki,
Na kumtumaini BWANA.
6 # Zab 80:3 Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mema?
BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.
7Umenitia furaha moyoni mwangu,
Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
8 # Law 26:5; Kum 12:10; Yn 14:27; Flp 4:7 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,
Maana Wewe, BWANA, peke yako,
Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia