Zab 6
SUV

Zab 6

6
Sala ya Kuponywa Ugonjwa Hatari
Kwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi; kulingana na mtindo wa Sheminithi. Zaburi ya Daudi.
1 # Zab 38:1 BWANA, usinikemee kwa hasira yako,
Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2 # Hos 6:1 BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;
BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3 # Mit 18:14; Mt 26:38 Na nafsi yangu imefadhaika sana;
Na Wewe, BWANA, hata lini?
4BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5 # Zab 30:9 Maana mautini hapana kumbukumbu lako;
Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6Nimechoka kwa kuugua kwangu;
Kila usiku nakieleza kitanda changu;
Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7Jicho langu limeharibika kwa masumbufu,
Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8 # Mt 7:23; Lk 13:27 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;
Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
9 # Zab 3:4; 31:22; 40:1,2 BWANA ameisikia dua yangu;
BWANA atayatakabali maombi yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia