Zab 61
SUV

Zab 61

61
Hakikisho la Ulinzi wa Mungu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Ya Daudi.
1Ee Mungu, ukisikie kilio changu,
Uyasikilize maombi yangu.
2 # 1 Tim 2:8 Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo,
Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
3 # Mit 18:10 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu,
Ngome yenye nguvu adui asinipate.
4 # Zab 15:1; 23:6; Ufu 3:12 Nitakaa katika hema yako milele,
Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako
5 # 1 Kor 3:21-23 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu.
Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.
6Utaziongeza siku za mfalme,
Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
7 # Zab 41:12; Lk 1:32 Atakaa mbele za Mungu milele,
Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.
8 # Zab 56:12 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima,
Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

Learn More About Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia